Nyimbo Mpya: Lava Lava 'Inatosha', Maua Sama 'Zai' na Ngoma Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba imeshawadia na ngoma ambazo zimetoka kwa hapa nchini Tanzania ni za kutosha sana. Makala hii imelenga kukupitisha kwenye ngoma kali ambazo zinafanya vizuri kwenye mtandao wa Youtube kwa wiki hii nchini Tanzania.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Video ya Ngoma Yake 'Inatosha'

Baba - Ney Wa Mitego ft Mtafya

"Baba" ya Ney Wa Mitego imeendelea kufanya vizuri na katika ngoma hii Ney anafunguka kuhusu mambo mbalimbali yanayotokea Tanzania kwa sasa kama ishu ya wamachinga, kesi za kisiasa na mambo mengine na kwenye mtandao wa Youtube ngoma imeshatazamwa takribani mara laki tatu

https://www.youtube.com/watch?v=_11TVmqd4is

Zai - Maua Sama

Video ya "Zai" kutoka kwa Maua Sama inaaendelea kufanya vizuri na hii ni kutokana na ubunifu ulikuwepo, stori nzuri ya kusisimua pamoja na kumtumia Hakika Reuben kama mhusika katika video hii imechangia kwa kiasi video hii kupendwa na mashabiki na kufikia sasa kwenye mtandao wa Youtube imeshatazamwa mara laki nne na saba.

https://www.youtube.com/watch?v=MAmFhxxGJoc

Oya Oya - Ali Kiba

Kutokea King's Music, Alikiba ameendelea kufanya vyema Youtube na video yake ya "Oya Oya" ambayo imefanyika huko kwa Madiba yaani Afrika Kusini chini ya usimamizi wa Director Kyle White na kufikia sasa ngoma hiyo imeshatazamwa mara Milioni mbili laki tisa kwenye mtandao wa Youtube

https://www.youtube.com/watch?v=HiX-aYj2yas

Inatosha - Lavalava

Stori nzuri, uhalisia pamoja na ufundi aliouonessha Hanscana kwenye video hii ya "Inatosha" ya kwake Lavalava ni moja ya vitu vichache ambavyo vimefanya video kupendwa sana na kufikia sasa imeshatazamwa mara laki tatu thelathini na nne kwenye mtandao wa Youtube 

https://www.youtube.com/watch?v=xlkwRl4tPhQ

Tamu - Mac Voice ft Rayvanny

Kwa wiki ya 3 mfululizo "Tamu" ya Mac Voice imeendelea kuwepo kwenye orodha ya nyimbo zinazofanya vizuri sana Youtube na kufikia sasa video ys ngoma hii ambayo imeandaliwa na Eris Mzava imeshatazamwa mara Milioni 2 laki mbiili kwenye mtandao wa Youtube 

https://www.youtube.com/watch?v=3mlDNZRkX6I

Leave your comment