Nyimbo Mpya: Rayvanny ‘New Chui’ EP, Alikiba ‘Bwana Mdogo’ na Ngoma Zingine Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

[Picha: Pulse Live]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Linapokuja suala la kutoa ngoma kali, basi wasanii kutokea nchini Tanzania huwa na umakini wa hali ya juu, na kwa wiki hii, kama ilivyo ada, wasanii kutokea Tanzania wameendelea kutoa ngoma na kanda za muziki ambazo zimepeperusha vyema bendera ya Bongo Fleva.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava 'Inatosha', Maua Sama 'Zai' na Ngoma Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii

Zifuatazo ni ngoma tano mpya kali ambazo zimeachiwa na wasanii kutokea Tanzania kwa wiki hii”

Bwana Mdogo - Alikiba ft Patoranking

‘Bwana Mdogo’ ni ngoma namba tisa kutoka kwenye albamu yake ya ‘Only One King’. Wiki hii Alikiba aliachia video ya ngoma hiyo ambayo imefanyika huko visiwani Zanzibar chini ya usimamizi wa Director Kylie White. Kufikia sasa video hio imeshatazamwa mara laki tano sabini na mbili kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=VvyDRDO6RLA

Soma Pia: Nyimbo Tano Bora za Hip-hop Kutokea Bongo Zinazogusia Suala la Pesa

Nay Wa Mitego - Baba 

Ney Wa Mitego ameendelea kuwa kipaza sauti cha watanzania. Ndani ya ngoma hii, anagusia amegusia masuala tofauti tofauti yanayoendelea Tanzania kama kesi za kisiasa, sakata la wamachinga na vitu vingine vingi ambavyo vinagusa watanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=_11TVmqd4is

Amsha Popo – Shilole

Baada ya ukimya wa takriban miezi kumi, hatimaye Shishi amerudi na ‘Amsha Popo’, ngoma ambayo ni moto wa kuotea mbali. Ndani yake anapeleka ujumbe mchungu kwa wote wanaopenda kumsema vibaya na wanaotumia jina lake kwa ajili ya kutafuta kiki.

https://www.youtube.com/watch?v=XqQKyV_y2N4

I Wish - Kusah

Kusah ameendelea kuonesha talanta yake ya uandishi pamoja na sauti nzuri ya kuimba kupitia ngoma yake mpya ya ‘I Wish’. Kusah alivuta umakini wa mashabiki kupitia video ya ngoma hii ambayo imesheheni watu maarufu tofauti tofauti kutokea Tanzania kama Wema Sepetu, Martin Kadinda Shilole, Petit Man na wengineo wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=vjxq0mREBy8

New Chui (EP) - Rayvanny

Kama ulidhani kuwa Rayvanny alimaliza kila kitu kwa mwaka huu baada ya kutoa albamu yake ya ‘Sounds from Africa’, basi habari ni kuwa bosi huyo wa Next Level ameachia EP ya kuitwa ‘New Chui’. ‘New Chui’ ni EP iliyoshonwa na ngoma sita za moto ambazo ni ‘Baila’, ‘Come’, ‘One Two’, ‘Party’, ‘Rare’, pamoja na ‘Stay’ aliyofanya na Abby Chams.

https://www.youtube.com/watch?v=HhYpk08eWik

Wasanii wengine waliotoa ngoma ni pamoja na Malkia Karen ‘Haja’ pamoja na Ibrah Nation ‘Somebody’.

Leave your comment