Nyimbo Mpya: Nandy ft. Marioo ‘Kufuli’, Mbosso ft. Zuchu ‘For Your Love’ na Ngoma Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

[Picha: Tuko]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mambo yanaendelea kuwa sukari kwenye kiwanda cha muziki nchini Tanzania, kwani wasanii wengi wameendelea kutoa ngoma mpya ambazo bila shaka zinakosha mashabiki. Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka nchini Tanzania kwa wiki hii:

Soma Pia: Lava Lava Azungumzia Wasanii wa WCB Kushindanishwa Miongoni Mwao

Kufuli - Nandy ft Marioo

‘Kufuli’ ni ngoma mpya kutoka kwa Nandy akimshirikisha Marioo. Kwenye ngoma hii Nandy anamsihi mpenzi wake abaki na yeye na asithubutu kumlaghai kwani ataumia sana.

https://www.youtube.com/watch?v=r9cJM9lAgFU

For Your Love - Mbosso ft Zuchu

Baada ya ‘Ashua’ kufanya vizuri, kwa mara nyingine tena Mbosso na Zuchu wanaileta ‘For Your Love’, ngoma ambayo Zuchu anatumia sauti yake nzuri kuonesha upendo alionao kwa mpenzi wake, huku Mbosso akiimba kwenye aya ya pili kukoleza ujumbe huo wa Zuchu.

https://www.youtube.com/watch?v=RXkmP1SbY28

Utamu - Mabantu

Mabantu wamerudi tena na ngoma yao mpya kabisa inayoitwa ‘Utamu’. Kwenye ngoma hii Mabantu wametumia lugha ya picha kuelezea vitu ambavyo mtu akivifanya vinapunguza utamu au hari ya kufanya jambo Fulani.

https://www.youtube.com/watch?v=1CifkGPWuU8

High School - Harmonize

Hatimaye wiki hii mwanamuziki Harmonize aliachia albamu yake iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu sana ya ‘High School’. Albamu hiyo imesheheni ngoma 20 huku ikishirikisha wasanii kama Ibraah, Anjella, Patoranking, Sholo Mwamba na Sarkodie.

https://www.youtube.com/watch?v=mPVoKSc6LJo

Jela - Ruby

Jela ni ngoma ambayo Ruby anaimba kwa hisia sana akionesha namna ambavyo kukosa pesa kunaweza kusababisha mtu ajihisi yuko ‘Jela’.

https://www.youtube.com/watch?v=eBLRIJQjpJE

Leave your comment