Lava Lava Azungumzia Wasanii wa WCB Kushindanishwa Miongoni Mwao

[Picha: Lava Lava Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki kutoka bongo Lava Lava amefunguka kuhusu madai ya wasanii wa lebo ya WCB kushindanishwa miongoni mwao.

Akizungumza wakati wa mahojiano na mtangazaji wa Kenya Presenter Ali, Lava Lava alisema kuwa suala la wanachama wa WCB kushindanishwa ni jambo nzuri. Alieleza kuwa wao kushindanishwa miongoni mwao kuna maanisha kuwa hakuna washindani wao ambao wamefikia kiwango cha ubora walichokifikia.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia ‘For Your Love’ Akimshirikisha Zuchu

''Ile naipenda kidogo kwa sababu wamekosa wa kutushindanisha nao. Unajua mpaka kushindanishwa na nyinyi wenyewe ina maana kuwa huko nje wamekosekana, so inaonyesha nyinyi ni wakubwa kiasi gani,'' Lava Lava alieleza.

Lava Lava pia alitoa kauli yake kuhusu lebo ya Konde Music Worldwide ambayo inamilikiwa na msanii nyota Harmonize. Harmonize alikuwa mwanachama wa zamani wa lebo ya WCB kabla kuiaga lebo hiyo na kuanza safari yake upya kupitia lebo yake binafsi.

Jambo hili lilionekana kuleta utofauti mkubwa baina yake na lebo ya WCB ambayo ndio ilimtoa na kumpa umaarufu. Kulingana na Lava Lava, ili tasnia ya muziki nchini Tanzania ikuwe, basi wanahitaji mchango wa kila msanii.

Soma Pia: Director Kenny Adhibitisha Kuondoka Kampuni ya Zoom Extra Inayomilikiwa na Diamond

Alisema kuwa uwepo wa Konde Gang pia unachangia katika kukuza tasnia ya muziki.

''Ili industry yetu ikuwe inabidi wasanii tukutane tuwe wengi. Na muziki ili upushiwe ndio ufike mahali unatakiwa kufika, inatakiwa pia watu wengine wawepo. So sio poa kwa kuzungumzia sana lakini ni sawa,'' Lava Lava alisema.

Lava Lava aliweka wazi kuwa kwa sasa anashughulikia utengenezaji wa albamu yake, jambo ambalo pia lilikuwa limemfanya kusafiri hadi nchini Kenya.

Leave your comment