Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia ‘For Your Love’ Akimshirikisha Zuchu

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya WCB Mbosso ameachia wimbo mpya aliyoipa jina la ‘For Your Love’ ambayo amemshirikisha Zuchu.

‘For Your Love’ ni wimbo mzuri wa mapenzi ambao ndani yake Zuchu na Mbosso wanachukua zamu kuambiana ukweli kwa namna gani wanapendana kwa dhati, huku kila mtu akionesha ni kwa namna gani anamuhitaji mwenzake kwenye maisha yake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia ‘High School’ Album

Zuchu anafungua ngoma hii kwenye aya ya kwanza kwa kutumia lugha ya kiingereza akiimba "Its the smile for me when you wake up in the morning mpenzi wangu. You touch me slowly nacheka cheka mwenzio you keep me falling mpenzi wangu."

‘For Your Love’ ni ngoma ya pili kutoka kwa Mbosso na Zuchu kwani ngoma ya kwanza kwa wasanii hao kufanya pamoja ni ‘Ashua’ ambao ulikuwa ni wimbo unaopatikana kwenye EP ya Zuchu ya ‘I am Zuchu’.

Soma Pia: Mimi Mars Atangaza Ujio wa EP Mpya Hivi Karibuni

‘For Your Love’ imetayarishwa na Mocco Genius ambaye pia alihusika kutayarisha ‘Ashua’ pamoja na ‘Cheche’ ambayo Zuchu alifanya na Diamond Platnumz, huku Lizer Classic kutokea Wasafi Records akihusika katika maandalizi ya mwisho ya wimbo huu.

Wimbo huu ni ngoma ya kwanza kutoka Mbosso kwa mwaka huu nje ya albamu ya ‘Definition of Love’ ambayo ilitoka mwanzoni mwa mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=RXkmP1SbY28

Leave your comment