Mimi Mars Atangaza Ujio wa EP Mpya Hivi Karibuni

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Mimi Mars amerudisha tabasamu kwa mashabiki zake baada ya kutangaza kuwa yuko mbioni kuachia EP yake mpya siku za hivi karibuni.

Mimi Mars ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani akiwa ameenda kumjulia hali dada yake Vanessa Mdee, alitoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo alichapisha picha na kuandika "EP mpya soon otea producer ni nani?"

Soma Pia: Mimi Mars Ajibu Tetesi za Kutopewa Thamani Kwenye Muziki wa Bongo Fleva

EP hii mpya kutoka kwa Mimi Mars inatarajiwa kuwa ni ya pili kutoka kwake. Mwaka 2018, alikuwa msanii wa kwanza kutokea Tanzania kuachia EP baada ya kuachia The Road EP ambayo ilisheheni ngoma sita.

Ngoma zilizounda The Road EP kutoka kwa Mimi Mars ni pamoja na ‘Mdogo Wangu’ aliyomshirikisha Nikki wa Pili, ‘Mua’, ‘Niache’, ‘Niguse’ pamoja na ‘One Night’ ikiwa ni EP ambayo ilifanya vizuri sana.

Soma Pia: Harmonize Adokeza Ujio wa Ngoma Mpya ya Singeli ya Kiingereza

Mara ya mwisho kwa Mimi Mars kutoa ngoma ilikuwa ni miezi mitatu liyopita alipoachia ngoma yake ya kuitwa ‘Zipo’ ambao ni wimbo maalum kwa ajili ya kuhamasisha watu watumie mitandao ya kijamii vizuri.

Pamoja na kukaa kimya kwa miezi hiyo mitatu, hivi karibuni Mimi Mars amekuwa akishirikishwa na wasanii wakubwa kama vile AY kwenye ‘Stakaba’, ‘Imooo’ ya Frida Amani pamoja na ‘Shindulia Chini’ ya Dogo Janja.

Leave your comment