Mimi Mars Ajibu Tetesi za Kutopewa Thamani Kwenye Muziki wa Bongo Fleva

[Picha: Mimi Mars Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Instagram

Mwimbaji tajika kutoka Tanzania Mimi Mars amekuwa kwenye darubini ya mashabiki walio hoji ni kwanini mwimbaji huyo hajakuwa alipewa thamani yake katika mziki wa bongo.

Hivyo wanashanga ni kwa nini kazi za gwiji huyu hazipati umaarufu japo ni mojawapo ya wasanii wakubwa kutoka Tanzania.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mimi Mars Aaachia Video Mpya ‘Wenge’

Shabiki mmoja kupitia mtandao wa Instagram aliuliza haswa ni kwa nini mwimbaji huyo hapewi heshima na thamani.

Akizungumza katika mahojiano, Mimi Mars alijibu swali hilo akisema kuwa ni kweli mashabiki wanachagua wasanii wa kuwasapoti lakini wengine hawapewi nafasi kama wasanii wengine.

Download Mimi Mars Music for Free on Mdundo

“Watanzania wanachagua wasanii, wakiamua kumchagua mtu au msanii fulani basi anakuwa huyo huyo, sisi wengine hatupewi nafasi kivile kama wengine. Kwani majority yao watawangalia hao wengine tu kama wasanii wetu, hivyo sisi wengine hatuonekani sana ila wachache ndio wanatutambua…” alisema Mimi Mars

Mwimbaji huyo wa ‘Haina Maana’ alisisitiza kuwa mfumo wa mziki umetenga wasanii fulani tu wakushabikiwa na wanepewa kipaumbele huku wengine wakijitahidi kuendeleza kazi zao.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Country Wizzy Aachia Video Mpya Kwa Jina ‘Baby’

Mars aliongeza kuwa ikiwa tu mfumo huo ungeunda usawa katika tasnia ya muziki, basi wasanii wengi kama yeye watafanikiwa.

Hivi karibuni Mimi Mars aliachia wimbo wake mpya wa ‘Wenge’ ambao haukupokelewa kwa kishindo ilivyotarajiwa. Kufikia sasa video ya wimbo huo in watazamaji zaidi ya elfu arobaini na mbili kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=ZGVxGjGp7Gg

Leave your comment