Nyimbo Mpya: Country Wizzy Aachia Video Mpya Kwa Jina ‘Baby’

[Picha: Country Wizzy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka lebo ya Konde Music Worldwide Country Wizzy ameachia kanda ya wimbo wake mpya kwa jina ‘Baby’.

Huu ni wimbo wa mapenzi ambapo Country Wizzy anamuahidi mpenzi wake mapenzi ya dhati na mazuri yote yanayoambatana na upendo.

Katika mistari ya wimbo huu tunaona Country Wizzy akifanya kuimba tofauti na anavyojulikana kama msanii wa Hip-hop.

Soma Pia: Playlists 5 Moto za Bongo Kwenye Mdundo Tanzania

“Vacay its Okay,Tell me baby Tukale bata S.A Au Zenji baby Mi nawee, Everywhere Aau kwenye boat meib… Believe Me It Feels so Good Yeah,Yeah Ukiwa Around me Ma’ It Really Feels So Good Yeah,Yeah Yo Body Around Me So Siwezi Kwenda Far Away (Far)….” Hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huu.

Download Country Boy Music for Free on Mdundo

Kanda hii imeaandaliwa kwa ujuzi mkubwa sana na wahusika wakuu wakiwa yeye tu na mrembo anaecheza sehemu ya ‘Baby’ wake.

Kwenye video, Country WIzzy na vixen huyo wanonekana wakiwa kwenye maandhari ya pwani wanapostarehe kwenye boti.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zinazotamba Mdundo Tanzania [Video]

Mdundo wa wimbo huu ulitengezwa na producer Ammy Wave na video ikiongozwa na mtayarishaji Elvis wote kutoka Tanzania.

Kufika sasa, kanda hii inaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube ikiwa na watazamaji zaidi ya laki moja.

https://www.youtube.com/watch?v=VR9I4EqyROI&feature=youtu.be

Leave your comment