Playlists 5 Moto za Bongo Kwenye Mdundo Tanzania

[Picha: Ghetto Radio]

Mwandishi: Omondi Otieno

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Mziki mzuri husaidia kutuliza akili na kuimarisha tija kazi. Unapoanza mwezi mpya na wiki mpya, ni muhimu kuanza na mziki mzuri utakao kupa motisha.

Kwenya nakala hii, tunaangazia playlists 5 kali kwenye mtandao wa Mdundo Tanzania zilizo na ngoma kubwa kubwa zinazofanya vyema Bongo na zilizochangwa na Ma DJs tajika.

Soma Pia: Nyimbo Tano za Rayvanny Zilizompa Umaarufu Bongo

Hii hapa orodha hio:

Bongo Flava Mix

Playlist hii ina mchanganyiko wa nyimbo zote mpya kutoka Bongo. Wasanii walioshirikishwa kwenye playlist hii ni kama vile; Diamond, Harmonize, Alikiba, Rayvanny, Zuchu, Mbosso, Nandy, Darassa, Lava Lava na wengine wengi. Hapa ndipo utapata ngoma zote moto nchini Tanzania, na uzuri ni kuwa haulipishwi chochote kusikiza au kupakua ngoma hizo. Mix hizo zinapatikana kwenye ukurasa huu: https://mdundo.com/p/23514

Singeli Mpya

Singeli ni aina ya mziki unaotumia sana za kitambo katika midundo yake. Kwa kuwa Mdundo inadhamini aina zote za muziki, playlist hii imetengezwa kuhakikisha unapata Singeli moto moto kutoka Tanzania mahali pamoja. Wasanii walioshirikishwa kwenye playlist hii ni kama vile; Meja Kunta, Dulla Makabila, Harmonize, Lava Lava na wengine wengi. Ili kusikiliza mix za Singeli kweye mtandao wa Mdundo, tembelea kurasa hii: https://mdundo.com/p/14846

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Zinazotamba Mdundo Tanzania [Video]

Nyimbo za Kuabudu

Mixtape hii ina mchanganyiko wa nyimbo moto moto za sifa na kuabudu kutoka nchini Tanzania na eneo la Afrika Mashariki. Wasanii walioshirikishwa ni kama vile; Christina Shusho, Martha Mwaipaja, Bahati Bukuku na wengine wengi. Unapohitaji kusikiliza nyimbo za kuabudu, tembelea ukurusa huu kwenye mtandao wa Mdundo: https://mdundo.com/p/14349

Taarab Starz

Hii ni mkusanyiko wa ngoma za Taarab zote zinazotamba nchini Tanzania. Mixtape hii imewashirika wasanii tajika wa Taarab kama vile; Bi Khadija Kopa, Khadija Yusuf, Leila Rashid, Ashira Machupa, Isha Mashauzi na wengine wengi. Ili kusikiliza na kupakua wimbo hizi bure, tembelea ukurusa huu: https://mdundo.com/p/20145

Waah! Diamond

Hii ni mixtape iliyo na mchanganyiko wa nyimbo bora kutoka kwa msanii tajika Diamond Platnumz. Orodha hii ina nyimbo kali kali kama vile; Waah aliyomshirika Koffi Olomide. Playlist hii pia ina mchanganyiko wa wimbo kutoka kwa maDJ tajika. Ili kuskiza ngoma zilizo kwenye playlist hii, tembelea ukurusa huu: https://mdundo.com/p/23236

Mixtape hizi tano ni miongoni mwa zingine mingi zilizo kwenye mtandao wa Mdundo. Ili kupata kuskiza playlists moto moto kutoka Tanzania, tembelea ukurusa huu: https://mdundo.com/playlists/tz. Iwapo unahitai kusikiliza mziki kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika, basi tembelea ukurusa huu: https://mdundo.com/genres/245.

Leave your comment