Harmonize Adokeza Ujio wa Ngoma Mpya ya Singeli ya Kiingereza
3 November 2021
[Picha: The Citizen]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mwanamuziki Harmonize ameendelea kuonesha ufundi na ubunifu kwenye muziki baada ya kuwapa mashabiki kionjo cha ngoma yake ambayo ina vionjo vya muziki wa Singeli.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram upande wa Instastory, Harmonize aliweka kipande cha wimbo huo ambao una mahadhi ya Singeli na kikubwa kuliko vyote ni kwamba ameimba kwa kutumia lugha ya kiingereza.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Ngoma Mpya ‘Wishes’
Kilichovuta umakini mkubwa wa mashabiki ni suala la Harmonize kuimba singeli kwa kiingereza; kitu ambacho mwanamuziki Kinata MC alishawahi kufanya kupitia ngoma yake ya ‘Do Lemi Go’ aliyofanya na Ibraah.
Aidha, Harmonize pia sio mgeni kwenye suala zima la kufanya muziki wa aina hiyo, kwani mwezi Februari mwaka 2020, Harmonize aliachia wimbo wa singeli wenye jina ‘Hujanikomoa’.
Kwa sasa, Harmonize yuko nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki. Itakapofika tarehe tano mwezi Novemba, Harmonize anatarajiwa kuachia albamu yake ya pili ya kuitwa ‘High School’.
Soma Pia: Harmonize Akana Kushiriki Kwenye Tuzo za AEAUSA Licha ya Kuteuliwa
Ili kuwatayarisha mashabiki kwa alabamu hiyo, harmonize ameachia wimbo mpya wenye jina ‘Wishes’.
‘Wishes’ si mojawapo ya ngoma zilizoko kwenye albamu hio inayosubiriwa kwa hamu.
Sikiliza Kionjo cha wimbo huo hapa chini kupitia kanda hii ya Mnazi TV.
Leave your comment