Harmonize Akana Kushiriki Kwenye Tuzo za AEAUSA Licha ya Kuteuliwa

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota Harmonize amekana kushiriki katika tuzo zozote siku chache baada ya kutajwa kama mmoja wa wasanii walioteuliwa kuwania tuzo za AEAUSA.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Harmonize aliwasihi wafuasi wake kutoharibu muda wao kumpigia kura kwani hayupo kwenye tuzo zozote.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Ngoma Mpya ‘Wishes’

Haijulikani hadi sasa sababu kuu iliyomfanya 'Teacher' kujiondoa kwenye tuzo alizotajwa. Swali ambalo limekosa jibu ni kwa nini Harmonize kuzikana tuzo za kifahari ambazo zimewahusisha wasanii wakubwa wakiwemo Alikiba, Diamond Platnumz na wengineo wengi.

''Am not nominated to any award, so please don't waste your bando, Kondegang F.C only,'' chapisho la Harmonize mtandaoni lilisomeka.

Soma Pia: Wasanii 5 Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Oktoba, 2021

Harmonize hapo awali alikuwa ameteuliwa kuwania tuzo za AEAUSA katika kitengo cha msanii bora Afrika Mashariki. Jumla ya wasanii kumi na mmoja kutoka Tanzania walitajwa kwenye uteuzi wa tuzo hizo katika vitengo mbali mbali.

Kauli ya Harmonize imeibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki na wadau wengine katika tasnia ya muziki ya Tanzania. Kando na taarifa hiyo ya Harmonize kukana tuzo alizoteuliwa ndani, kwa sasa msanii huyo ni gumzo mtandaoni kutokana na albamu yake ambayo inatarajiwa kutoka mnamo tarehe tano mwezi huu.

Albamu hiyo iliyopewa jina la 'High School' iko na jumla ya ngoma ishirini. Harmonize vile vile ameachia wimbo mpya kwa jina la 'Wishes'.

'Wishes' kufikia sasa imetazamwa takriban mara laki moja kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment