Wasanii 5 Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Oktoba, 2021

[Picha: PPP]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwezi Novemba umeshatimia, na kama kawaida kila mwezi mtandao wa Chart Data hutoa orodha ya wasanii ambao ndani ya mwezi husika wametazamwa zaidi YouTube.

Hivyo basi, hawa hapa ni wasanii watano kutoka Tanzania waliotazamwa zaidi YouTube kwa mwezi Oktoba 2021.

Soma Pia: Alikiba, Zuchu, Nandy, Diamond, Harmonize, Rayvanny, Macvoice na Wengineo Wachaguliwa Kuwania Tuzo za AEAUSA

Diamond Platnumz

Kwa mara nyingine tena Diamond Platnumz ameongoza kwa kutazamwa zaidi YouTube. Mwezi Oktoba pekee, video za kwenye akaunti yake zilitazamwa mara milioni 33.6 na pia ndani ya mwezi huo, aliachia ngoma yake ya ‘Gimmie’ aliyofanya na Rema.

Rayvanny

Rayvanny kwa mwezi Oktoba anashikilia nafasi ya pili kwani alitazamwa mara milioni 20.9 huko YouTube. Ikumbukwe kuwa ni ndani ya mwezi Oktoba ndipo Chui aliachia EP yake ya ‘New Chui’ ambayo inatamba kwa sasa.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny ‘New Chui’ EP, Alikiba ‘Bwana Mdogo’ na Ngoma Zingine Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Alikiba

Alikiba kwa mwezi Oktoba alitazamwa mara milioni 13.6 kwenye akaunti yake ya YouTube. Kutazamwa huku kulichangiwa sana na albamu yake ya ‘Only One King’ ambayo iliachiwa Oktoba 7 na kupokewa vizuri na mashabiki.

Harmonize

Imepita takriban miezi miwili tangu Harmonize aachie ngoma yoyote lakini hiyo haijamzuia ‘Teacher’ kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube. Ndani ya mwezi Oktoba, ametazamwa mara milioni 11.8 na kushika nafasi ya nne.

Zuchu

Zuchu anashika nafasi ya tano kwenye orodha hii akiwa ametazamwa mara milioni 11.4 kwenye akaunti ya YouTube. Kwa mwezi Oktoba, Zuchu alishirikiana na Spice Diana kwenye ngoma ya ‘Upendo’ ambayo ilifanya vizuri.

Leave your comment