Alikiba, Zuchu, Nandy, Diamond, Harmonize, Rayvanny, Macvoice na Wengineo Wachaguliwa Kuwania Tuzo za AEAUSA

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Waandaaji wa tuzo za Africa Entertainment Awards USA (AEAUSA) wametangaza orodha ya wasaniii ambao wamechaguliwa kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu wa 2021.

Habari njema ni kuwa wanamuziki 11 kutokea Tanzania wametangazwa kuwania tuzo hizo. Mmoja ya wasanii hao ni Mac Voice ambaye ana mwezi mmoja tu tangu atambulishwe, amechaguliwa kuwania kipengele cha msanii bora chipukizi barani Afrika akishandana na wasanii kama Omah Lay, Ayra Starr, Liya na wengineo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny ‘New Chui’ EP, Alikiba ‘Bwana Mdogo’ na Ngoma Zingine Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Diamond Platnumz amechagulia kuwania vipengele vitano ambavyo ni msanii bora wa mwaka, msanii bora wa kiume huku ngoma yake ya ‘Waah’ ikiwa inawania nafasi ya wimbo bora wa kushirikiana, wimbo bora wa mwaka na video bora ya mwaka.

Wasanii wengine kutoka WCB waliopata uteuzi kwenye tuzo hizo ni pamoja na Zuchu ambaye anawania kipengele cha msanii bora wa kike kutokea Afrika akichuana na Tiwa Savage, Yemi Alade na Nandy pamoja.

Zuchu pia meteuliwa kwenye kikundi cha msanii bora wa kike Africa Mashariki, Kusini na Kaskazini mwa Afrika kipengele ambacho pia anachuana na Nandy.

Alikiba amechaguliwa kuwania tuzo ya msanii bora wa Afrika Mashariki huku ngoma yake ya ‘Salute’ ikipambana katika sehemu ya video bora ya mwaka.

Soma Pia: Nyimbo Tano Bora za Hip-hop Kutokea Bongo Zinazogusia Suala la Pesa

Harmonize ameteuliwa kuwania tuzo ya msanii bora Afrika mashariki. Kundi la Navy Kenzo pamoja na Weusi wameteuliwa kuwania kama kundi bora la mwaka.

Rayvanny amelamba teuzi katika vipengele vinne ambavyo ni msanii bora Afrika Mashariki, ngoma yake na Zuchu ‘Number One’ imeteuliwa kama video bora ya mwaka, na wimbo bora wa mwaka. Albamu yake ya ‘Sounds From Africa’ na ‘Definition Of Love’ ya Mbosso zinawania albamu bora ya mwaka.

Upande wa Hip-hop wamewakilishwa na Rosa Ree ambaye anawania tuzo ya msanii bora wa Hip-hop. Mimi Mars anawania tuzo ya msanii anayekuja kwa kasi barani Afrika.

Tuzo za AEAUSA zinatarajiwa kufanyika mwezi Januari 2022. Mashabiki wanaweza wakapiga kura kupitia tovuti ya AEUSA.

Leave your comment