Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia ‘High School’ Album

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Harmonize hatimaye ameachia albamu yake mpya yenye jina ‘High School’.

‘High School’ ni albamu ambayo imesheheni ngoma ishirini, huku ikiwa imeshirikisha wasanii wa Tanzania kama Ibraah, Anjella pa; moja na Sholo Mwamba.

Soma Pia: Ibraah Apendezwa na ‘High School’ Album ya Harmonize, Aitaja Albamu Bora Afrika

Alabamu hio pia imeshirikisha wasanii kutoke nje ya Tanzania kama vile Busiswa pamoja na Sarkodie.

Kati ya ngoma ishirini zilizounda albamu hii, ni ngoma moja tu ya ‘Teacher’ ambayo tayari ilikuwa imeshatoka huku ngoma nyingine kama vile ‘Influencer’, ‘Sorry’, ‘Outside’, ‘Always’, ‘Turn Up’ na nyinginezo zikiwa ni ngoma mpya kabisa ambazo hazijawahi kusikika.

Albamu ya ‘High School’ imesheheni ngoma ambazo zina vionjo tofauti tofauti kwani kwenye ngoma kama ‘Sandakalawe Remix’ na ‘Teacher’ ameimba Amapiano, na kwenye ngoma kama ‘Muziki’ na ‘Kamaliza’ ameimba Singeli.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia EP Mpya ‘New Chui’

Ngoma nyingine za kwenye albamu hii ina vionjo vya Afro Pop na Bongo Fleva.

Albamu hii inakuja saa chache baada ya Harmonize kufanya listening party kupitia akaunti yake ya Instagram, ambapo alieleza kuwa kuna baadhi ya nyimbo kwenye albamu hiyo zinahusu maisha yake binafsi.

Kulingana na Harmonize, wimbo wa ‘Sorry’ ni maalum kwa ajili ya mke wake wa zamani Sarah.

Ikumbukwe hii ni albamu ya pili kutoka kwa Harmonize ambayo inakuja miezi ishirini baada ya ‘Afro East’ ambayo ilikuwa ni albamu yake ya kwanza.

Leave your comment