Ibraah Apendezwa na ‘High School’ Album ya Harmonize, Aitaja Albamu Bora Afrika

[Picha: Standard Media]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Ibraah kutokea himaya ya Konde gang amependezwa na albamu mpya ya Harmonize yenye jina ‘High School’ inayotarajiwa kuachiwa tarene tano Novemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa Ibraah, albamu hiyo ina viwango vya hali ya juu kiasi cha kuiita albamu hiyo mojawapo kati ya albamu bora kuwahi kutokea Afrika nzima.

Soma Pia: Ibraah Atangaza Tamasha Jipya ‘Ibraah Homecoming’

Muda mfupi baada ya Harmonize kuweka wazi kwamba Novemba 5 ndiyo tarehe rasmi atakayoachia albamu yake, Ibraah kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe huu: "Kwangu mimi hii ni moja ya albamu bora kuwahi kutokea Afrika na am so proud kuwa mmoja ya walioshirikishwa humu ndani."

Ibraah ameshirikishishwa kwenye ngoma namba kumi ya kuitwa ‘Mdomo’, ikiwa ni mara ya pili kwa wasanii hao kukutana kwenye ngoma tangu ilipotoka ‘One Night Stand’ mwezi Mei mwaka 2020.

Soma Pia: Ibraah Afichua Sababu ya Kumwacha Harmonize Marekani na Kurudi Tanzania

Ikumbukwe Ibraah nae kwa muda mrefu sasa ametangaza kuwa albamu yake imeshakamilika na yuko kwenye maandalizi ya kuiachia. Mwanamuziki Cheed pia aliungana na Ibraah katika kuonesha kuwa albamu hiyo ya Harmonize ni kali.

Cheed aliandika kuwa "Oyaah Run Away High School Is Coming. Fundi wa melodies Uandishi Harmonize Big Bro World Wide."

Cheed kwa sasa anatamba na ngoma yake ya ‘Final’ aliyoiachia hivi karibuni.

Leave your comment