Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia EP Mpya ‘New Chui’

[Picha: EA Feed]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Next Level Music Rayvanny ameachia EP mpya inayokwenda kwa jina la ‘New Chui’.

EP ya ‘New Chui’ imesheheni ngoma sita za moto ambazo ni ‘Come’, ‘Rara’, ‘Baila’, ‘One Two’, ‘Party’ pamoja na ‘Stay’ ambayo amemshirikisha mwanamuziki Abby Chams.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Video ya Ngoma Yake 'Inatosha'

Ngoma za kwenye EP hii zimetayarishwa na manguli wa muziki kutokea Tanzania kama S2kizzy, Lizer Classic kutokea Wasafi Records, Trone na Sound Boy aliyeshiriki kwenye kuaandaa ngoma ya ‘Party’ na ‘One Two’.

Kwenye EP hii, Rayvanny ameimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti kama vile Bongo fleva, RnB na Kizomba.

Kinachovutia zaidi ni namna ambavyo Rayvanny ameweza kuimba lugha ya kiingereza kwenye ngoma tofauti tofauti kwenye EP ikiwemo ‘Stay’ ambayo amefanya na Abby Chams.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video ya Wimbo wake wa Amapiano 'Beer Tamu'

‘New Chui’ ni EP ya pili kutoka kwa Rayvanny tangu aanze muziki na inakuja miezi takriban 18 tangu aachie EP yake ya ‘Flowers’, ambayo ilitikisa Tanzania nzima kwa mwaka 2020.

Huu umekuwa ni mwaka mzuri sana kwa Rayvanny. Ukiachilia mbali kuwa aliachia albamu yake mwanzoni mwa mwaka huu, pia ameweza kumtambulisha Mac Voice kama msanii wake wa kwanza kutoka kwenye lebo yake ya Next Level Music.

https://www.youtube.com/watch?v=SNkiwfedn7g

Leave your comment