Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video ya Wimbo wake wa Amapiano 'Beer Tamu'

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamziki kutoka Bongo Marioo hatimaye ameachia kanda ya wimbo wake wa Amapiano "Beer Tamu".

Kwenye "Beer Tamu" amewashirikisha Tyler ICU, Visca na Abbah Process.

Soma Pia: Marioo Atangaza Ujio wa Ziara Yake ya Muziki Nchini Tanzania

Video ya ‘Beer Tamu’ imejaa ubunifu wa aina yake na ina stori nzuri ambayo inachekesha.

Kinachovutia zaidi kwenye video hii ni pale ambapo baadhi ya wahusika wanavaa mavazi yanayofanana na mavazi waliovaa wahusika kwenye tamthiliya maarufu duniani kwa sasa ya ‘Squid Game’.

Soma Pia: Marioo Adhibitisha Ujio wa Kolabo Zake na Alikiba, Diamond Platnumz

Video ya ‘Beer Tamu’ imetayarishwa na mshindi wa tuzo ya Afrimma Director Kenny ambaye ameshafanya kazi na wasanii tofauti kutokea Tanzania kama Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Zuchu, Mbosso, Vanessa Mdee na wengine wengi.

‘Beer Tamu’ ni video ya tatu kutoka kwa Marioo kwa mwaka 2021. Kabla ya video hii, Marioo aliachia ‘For You’ iliyotayarishwa na Adam Juma pamoja na ‘Wow’ ambayo pia ilifanya vizuri nchini Tanzania.

‘Beer Tamu’ ni ngoma ya pili ya Amapiano kutoka kwa Marioo baada ya kuachia ‘Mama Amina’ mwishoni mwa mwaka jana.

https://www.youtube.com/watch?v=J5Ka53RZUtE

Leave your comment