Marioo Atangaza Ujio wa Ziara Yake ya Muziki Nchini Tanzania

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka Tanzania Marioo ametangaza ujio wa ziara yake ya muziki nchini humo kuanzia tarehe 30 mwezi huu.

Tamasha la kwanza kwenye ziara hiyo iliyopewa jina la 'I Am Marioo Tour' litafanyika mjini Mwanza katika eneo la burudani la Cask Bar.

Soma Pia: Marioo Adhibitisha Ujio wa Kolabo Zake na Alikiba, Diamond Platnumz

Hata hivyo, kulitokea mkasa wa kusikitisha ambapo eneo hilo la Cask Bar liliteketea kwa mkasa wa moto. Licha ya hili, Marioo ameisisitiza kuwa bado atawaburudisha mashabiki wake katika eneo hili hilo lililotekea.

Alisema kuwa hakuna chochote kitakachosimama mbele yake ata uwe huo mkasa wa moto. Wasanii wengi wakiwemo Maua Sama, Shetta, Mwana FA na wengine wengi walijitokeza na kumpongeza kwa ujasiri wake wa kutositisha ziara yake kwa sababu ya mkasa huo.

Read Also: Marioo Adai Yeye Ndiye Muanzilishi wa Swahili Amapiano

"Kweli @the_cask_bar Imeungua ila wamesema Hatupoi hatuboi Show letu tunalipiga kama kawa na kiwanja ni kile kile @the_cask_bar Mwanza Tunakutuna palipo ungua shoka na Mpini ukabaki #thecask #MariooTour #IMT tar30/10 Jumamosi hii sio ya kukosa," chapisho la Marioo mtandaoni lilisomeka.

Marioo kufikia sasa hajatoa ratiba kamili ya ziara yake na pia hajafichua iwapo atawahusisha wasanii wengine kwenye ziara hiyo. Tangazo hili linatokea muda mfupi baada ya Marioo kufichua kuwa kolabo baina yake na wasanii wakubwa Tanzania ambao ni Diamond Platnumz na Alikiba zipo njiani zaja.

Marioo ni mmoja wa wasanii wa bongo wenye ushawishi mkubwa sana na pia mwenye mafanikio.

Leave your comment