Marioo Adhibitisha Ujio wa Kolabo Zake na Alikiba, Diamond Platnumz

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Marioo amedhibitisha ujio wa kolabo baina yake na wasanii wawili wakubwa ambao wamedaiwa kuwa mahasimu wake kwa muda mrefu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, wakati anajibu maswali kutoka kwa mashabiki wake, Marioo alidhibitisha kuwa kazi baina yake na Diamond Platnumz na vile vile Alikiba zipo njiani.

Soma Pia: Marioo Adai Yeye Ndiye Muanzilishi wa Swahili Amapiano

Kwa mujibu wa Marioo, alikuwa amesubiri Alikiba atoe albamu yake ya ‘Only One King’ kabla ya kuingia studioni naye. Tayari Alikiba ashatoa albamu hiyo na hivyo basi huenda wawili hao wakaingia studioni muda wowote.

Alikiba hapo awali alisema kuwa kwa muda mrefu hajakuwa akifanya kolabo na wasanii wengine sana, ila kwa ajili ya mashabiki wake ameamua kuongeza idadi ya kolabo anazofanya.

Soma Pia: Marioo Atangaza Tarehe ya Kuachia Albamu Yake Mpya

Alishirikiana na wasanii mbali mbali kutoka sehemu tofauti ya bara la Afrika kwenye albamu yake ambayo imepokelewa vizuri na mashabiki.

Kwa upande mwingine Marioo anasubiri Diamond Platnumz arejee kutoka kwa ziara yake ya muziki Marekani kabla ya kushirikiana na yeye. Ziara ya Diamond Marekani imeratibiwa kukamilika mnamo tarehe 31 mwezi huu.

Diamond vile vile yupo Marekani kwa ajili ya albamu yake ambayo imesimamiwa na mtayarishaji wa muziki Swizz Beats. Msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya WCB bado hajaweka wazi iwapo atarejea nchini Tanzania pindi atakapomaliza ziara yake, ama atabaki marekani kwa muda kwa ajili ya albamu.

Kolabo baina ya Marioo na wasanii hawa wawili bila shaka itatetemesha anga za burudani kwani kando na yeye kuwa na ushwawishi mkubwa, atakua mmoja wa wasanii wachache ambao wamefanya kazi na Alikiba na Diamond Platnumz.

Leave your comment