Marioo Adai Yeye Ndiye Muanzilishi wa Swahili Amapiano

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Marioo amedai kuwa yeye ndiye muanzilishi wa mtindo wa muziki wa Swahili Amapiano. Katika chapisho alilolieka mtandaoni, Marioo alisema kuwa yeye ndiye alikuja na mtindo huo kabla haujapata umaarufu miongoni mwa wasanii wa bongo.

Mtindo wa Swahili Amapiano kwa siku za hivi karibuni umevuma sana nchini Tanzania huku wasanii tajika wakitunga nyimbo kutumia midundo hizo kutoka Afrika Kusini.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video ya ‘Wow’

Miongoni mwa wasanii wakubwa ambao wametoa nyimbo kwa mtindo wa Swahili Amapiano ni pamoja na Harmonize na Diamond Platnumz. Aidha kauli ya Marioo inatokana na sababu kuwa yeye alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kabisa nchini Tanzania kutunga ngoma ya Kiswahili kwa kutumia midundo za Amapiano.

Ngoma hiyo inayokwenda kwa jina la 'Mama Amina' ulipata umaarufu mkubwa sana na kutazamwa mara mingi katika mtandao wa YouTube. Kufikia sasa 'Mama Amina' ambayo pia iliwahusisha wasanii wa Afrika Kusini ikiwemo Sho Madjozi na Bontle Smith imetazamwa takriban mara milioni sita nukta nane.

Soma Pia: Marioo Atangaza Tarehe ya Kuachia Albamu Yake Mpya

Mario vile vile katika chapisho lake alidokeza kuwa hivi karibuni atakua anaachia ngoma nyingine mpya kwa mtindo huo huo wa Swahili Amapiano. Katika Ngoma hii mpya ameshirikiana na mtayarishaji wa miziki Tyler ICU kutoka Afrika Kusini.

"Me ndo niliyeileta hii #SwahiliAmapiano so kama hamuitaki tena Mnambie niirudishe kwaoSi et!! @tylericu Asking when should He drop this," chapisho la Mario lilisomeka.

Chapisho hilo lilivutia hisia mbali mbali huku DjJ maarufu Romy Jons kutoka lebo ya WCB akitoa kauli yake kwenye sehemu ya maoni ya chapisho hilo. "Wewe ndio umeleta kila kitu kaka angu," Romy Jons aliandika.

Leave your comment