Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video ya ‘Wow’

[Picha: CitiMuzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Marioo kutokea nchini Tanzania hatimaye ameachia video ya wimbo wake wa ‘Wow’.

Audio ya ‘Wow’ iliandaliwa na mtayarishaji wa muziki nguli kutokea Tanzania Kimambo beats na ilitoka Julai 30 mwaka huu.

Soma Pia: Amapiano: Mdundo Unaobadilisha Mitindo ya Muziki wa Bongo Fleva

Video ya ‘Wow’ inavuta umakini wa mtazamaji kuanzia mwanzo mpaka mwisho kwani video hiyo imepambwa na stori nzuri huku wadada warembo wakionekana kucheza kwa madoido mengi.

 Ndani ya video hiyo, watu maarufu kama mtayarishaji wa muziki Abbah Process ambaye ni rafiki mkubwa wa Marioo wameshirikishwa.

‘Wow’ imeongozwa na Director Ivan ambaye pia amehusika kuandaa video za wasanii wengine kama ‘Tout Le Monde’ ya Weusi, ‘Fimbo’ ya Weusi pamoja na ‘Mapepe’ ya Rayvanny.

Marioo siku ya jana alidokeza ujio wa video hiyo baada ya kuchapisha video kwenye akaunti yake ya Instagram ikimuonesha yeye na Abbah Process pamoja na Jux ndani ya boti na kusindikiza na ujumbe "General Abbah process ndo kashasema. King of hearts Juma Jux and Golden Boy Ciza SA they approved it as well so we good to go."

Kwa mwaka huu, hii ni video ya pili kutoka kwa Marioo baada ya kuachia video ya wimbo wake wa ‘For You’ April 8 mwaka huu na ilifanya vizuri sana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Wimbo Mpya wa Mapenzi ‘For You’

Aidha, Marioo Julai 15 mwaka huu alitangaza ujio wa albamu yake ambayo inatarajiwa kutoka Septemba 25 mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=HAB1rCi66ME

Leave your comment