Amapiano: Mdundo Unaobadilisha Mitindo ya Muziki wa Bongo Fleva
11 April 2021
[Picha: Sho Madjozi Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Tanzania inajulikana barani Afrika kwa muziki wake wa Bongo Fleva. Muziki huu una midundo ya kisasa na huwa umeandikwa kishairi kwa lugha ya Swahili.
Muziki wa Bongo Fleva umekua ukipitia mabadiliko iliyoletwa na teknolojia n ustadi wa waandalizi wa muziki kama vile S2kizzy, Ayo lizer, Producer Abbah na wengine wengi.
Soma Pia: Mafanikio 5 Kuu ya Zuchu Mwaka Mmoja Baada ya Kuzinduliwa na WCB
Kwa muda mrefu, Bongo Fleva imekua ikivuma nchini Tanzania huku wasanii wengine wakisimama na muziki huo licha ya aina zingine za muziki kuchipuka Afrika.
Hata hivyo, Afrika Kusini wametuletea mdundo mpya kwa jina Amapiano. Ikumbukwe kuwa Afrika Kusini imejitambulisha kama moja ya vituo kuu vya muziki wa nyumbani (AfroHouse) ulimwenguni, lakini katika muongo mmoja uliopita, tofauti ya aina hiyo imeibuka kutoka kwa miji ya Johannesburg na Pretoria na kupata umaarufu mkubwa katika mitindo ya muziki ulimwenguni.
Muziki wa Amapiano nao umepata mlipuko mkubwa mwaka huu 2021, dhihirisho la mabadiliko ya mtindo wa muziki wa Kiafrika. Hili likifuatia ubunifu mkubwa katika utandawazi haswa mfumo digitali na kuongezeka kwa mziki wa aina hii.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video Yake Mpya ‘For You’
Amapiano ni mziki wa kielektroniki unaochanganya Afro House pamoja na mitindo mingine maarufu katika miji ya Afrika Kusini, kama Jazz na Kwaito. Muziki huu ulipata umaarufu Ulimwenguni kupitia kwa wasanii kama vile DJ Maphorisa na Kabza De Small.
Kufikia sasa wasanii wa Bongo wameanza kufanya mziki kutumia mdundo huu ambao kwa sasa tunaeza sema kuwa umejipenyeza kwenye fani ya mziki wa Bongo.
SOma Pia: Rais Samia Suluhu Ashauri Serikali yake Kuzingatia Changamato za Wasanii
Hivi karibuni msanii kutoka Tanzania Marioo alishirikiana na Sho Madjozi kwa wimbo ‘Mama Amina’, vile vile Mbosso kwenye album yake ameweka “Kamseleleko” Harmonize na wimbo wake “Anajikosha” na wengine wengi.
Hivyo jinsi tulifurahia ujio wa Afro Beats kutoka Nigeria, Afrika Kusini nao pia wametangaza msimamo kwa sasa.
Leave your comment