Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Video Yake Mpya ‘For You’

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Bongo Marioo ameachia kanda ya wimbo wake mpya ‘For You’.

Marioo alishangaza mashabiki alivyobadilisha maudhui na kushabikia mapenzi. Kwanza kabisa Marioo anashangaa ni vipi hakujua uzuri ulioko kwenye mapenzi. Katika mistari yake anasema amejua kuwa hii dunia ni tamu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

“Hii dunia kumbe tamu, Ulikuwa wapi kuenjoy wanadamu, Yaani dunia kumbe tamu Ili nilikuwa wapi mmmh, We unanipatia maana nilishalalia sana, Navyojikatia tamaa, ooh lalalee…” aliimba Marioo.

Katika hali zake za kupagawishwa, Marioo anaonekana kupendezwa na binti mmoja mrembo. Wawili hao wanaonekana kufurahia wakati wao pamoja katika maeneo tofauti ya kujiburudisha.

‘For You’ imempa Marioo fursa ya kujiuza kama muimbaji wa utaofati na talanta kubwa sana. Kanda hii ina mandhari ya kupendeza huku Marioo akiomba kumuimbia mrembo huyo huku akimuahidi mapenzi ya dhati.

Soma Pia: Rosa Ree Azua Gumzo Baada ya Kuachia Wimbo Mpya ‘Satan’

Vile vile, mikato ya video hii imefanywa kwa ustadi mkubwa huku wahusika wakiwa Marioo na binti huyo mrembo.

Mdundo wa wimbo huu unaambatana na mdundo wa kizomba. Video hii ilitengezewa Zanzibar na mwelekezaji Adam Juma huku mdundo wa wimbo huu ukifanywa na Producer Abbah Process.

Kanda hii imepokelewa vizuri na mashabiki huku watazamaji wakiwa zaidi ya elfu thelathini na saba kwa sasa.

https://www.youtube.com/watch?v=e3Aym00lfB4&ab_channel=MariooOfficial

Leave your comment