Director Kenny Adhibitisha Kuondoka Kampuni ya Zoom Extra Inayomilikiwa na Diamond

[Picha: DK Limited Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Muongozaji wa video Director Kenny hatimaye amedhibitisha kuondoka kampuni ya Zoom Extra inayomilikiwa na mwanamuziki nyota Diamond Platnumz.

Kwa muda mrefu sasa Director Kenny amekua akiongoza utengenezaji wa video za wasanii wa WCB kupitia kampuni ya Zoom Extra.

Soma Pia: Dancer wa Diamond Angel Nyigu Azungumzia Uwezekano Wake Kufanya Kazi na Alikiba, Konde Gang

Tetesi, hata hivyo, ziliibuka mtandaoni wiki chache zilizopita kuhusu Director Kenny Kuondoka kampuni hiyo. Tetesi hizo zilitokana na Director Kenny kukosekana katika video za hivi karibuni za wasanii wa WCB.

Nafasi ya Director Kenny ilichukuliwa na Hanscana ambaye kwa sasa ndiye ametawala katika kusimamia video za wasanii wa WCB. Baada ya kubaki kimya kwa muda, Director Kenny hatimaye amedokeza hali ya uhusiano wake na kampuni ya Zoom Extra.

Director Kenny alibadilisha jina la ukurasa wa Instagram uliokuwa wa Zoom Extra na kulipa jina mpya la DK Limited (Director Kenny Limited).

Soma Pia: Diamond Asifia Wimbo wa ‘Inatosha’ Kutoka kwa Lava Lava

Hii imeashiria kuwa kando na yeye kuiaga Zoom Extra, ameanzisha kampuni yake binafsi ambayo pia inarekodi video za muziki. Katika chapisho alizoeka hivi karibuni kwenye ukurasa huo wa DK Limited, ni kazi ambayo amefanya na msanii Marioo kwenye video ya wimbo wa 'Beer Tamu'.

Hii imekuwa dhihirisho tosha kuwa kwa sasa Kenny anafanya kazi kama muongozaji wa video huru chini ya kampuni yake.

Haijulikani kilichomsukuma Director Kenny kutengana na Diamond Platnumz na hadi kuondoka kampuni ya Zoom Extra. Vile vile haijulikani iwapo kampuni ya Zoom Extra imekufa na kuondoka kwa Kenny au itafufuliwa upya.

Leave your comment