Diamond Asifia Wimbo wa ‘Inatosha’ Kutoka kwa Lava Lava

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki kutoka Tanzania Diamond Platnumz ameusifu wimbo wa ‘Inatosha'’ kutoka kwa msanii maarufu Lava Lava.

'Inatosha' ndio ngoma mpya kabisa kutoka kwa Lava Lava ambaye pia ni mwanachama wa lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Soma Pia: Wasanii 5 Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Oktoba, 2021

 Kupitia chapisho aliloliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diamond Platnumz alisema kuwa amependezwa na kazi ya Lava Lava. Alisistiza kuwa 'Inatosha' ndio ngoma bora ya kiafrika kwake kwa mwaka huu.

Aliwasihi wafuasi wake wakaenda wakapitie mistari ya ngoma hiyo iwapo wangetaka kufahamu mbona anaupenda sana.

''My current 2021 African Favorite tune for some Reason....Google the lyrics and translation, then you will know why,'' Diamond aliandika mtandaoni.

'Inatosha' ni wimbo ambao unazungmzia kauli ya mwimbaji kukata tamaa na mapenzi baada ya kupitia maumivu na ugomvi mwingi. Kupitia mistari ya wimbo huo, Lava Lava anasema kuwa upendo wa wazazi unatosha na hahitaji kuwa katika mahusiano ya kimapenzi.

Soma Pia: Alikiba, Zuchu, Nandy, Diamond, Harmonize, Rayvanny, Macvoice na Wengineo Wachaguliwa Kuwania Tuzo za AEAUSA

Ujumbe huu ni wa kipekee kwani Lava Lava anasifu umuhimu wa mtu kuwa pekee yake na uhuru unaotokana na kutokuwa katika mahusano.

Huenda ujumbe huu ndio ulimgusa Diamond Platnumz kwani siku chache hapo nyuma, Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema kuwa ni heri mtu kuongeza bidii katika kazi na kuacha mahusiano ya kimapenzi.

Ngoma hii, tofauti na ngoma mingi, imechanganya mtindo wa bongo na rhumba, kigezo ambacho pia kimewavutia wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=xlkwRl4tPhQ

Leave your comment