Dancer wa Diamond Angel Nyigu Azungumzia Uwezekano Wake Kufanya Kazi na Alikiba, Konde Gang

[Picha: Angel Nyigu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msakataji densi maarufu kutoka bongo Angel Nyigu amezungumzia kuhusu uwezekano wa kufanya kazi na wapinzani wa bosi wake Diamond Platnumz.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya wakati wa ziara yake nchini Kenya, Nyigu alisema kuwa iwapo nafasi itatokea ya kufanya kazi na wapinzani wa Diamond kama vile Alikiba na Harmonize, basi atalazimika kuikataa.

Soma Pia: Angel Nyigu Akerwa na Wasanii Wasiounga Mkono Wasakataji Densi

Alifafanua kuwa yeye hajihusishi na utofauti uliopo baina ya wasanii, ila kwa heshima ya kazi yake ndani ya lebo ya WCB, hawezikubali kushirikiana na wapinzani wa lebo hiyo.

Kwa sasa, Angel Nyigu anashikilia nafasi ya mwelekezaji wa densi wa malkia wa bongo Zuchu. Angel Nyigu, hata hivyo, aliongeza kuwa ashawahi fanya kazi na Harmonize kipindi alikuwa bado WCB kabla ya kuondoka na kuanzisha lebo yake.

Msakataji densi huyo aliashiria kuwa anafurahia kazi yake kwa sasa na nafasi aliyonayo. Hata hivyo, Angel Nyigu alikiri kuwa huenda uamuzi wake ukawafanya baadhi ya mashabiki kumwona vibaya. Ila kwa haraka aliongezea kuwa yeye hapendi kuishi maisha bandia au ya uongo na ndio maana akasema ukweli wa msimamo wake.

“Nishawahi fanya kazi na Harmonize akiwa WCB. Mimi sipo katika hizo mashida zao, mashida zao mimi sipo, hainihusu. To be honest, I dont sijui watu wengi wanaweza wakani picture vibaya, lakini I can’t,” Angel Nyigu alisema.

Soma Pia: Maua Sama Azungumzia Uhusiano Wake Na Nandy

Angel Nyigu kwa sasa yupo nchini Kenya ambako amekutana na wasakataji densi maarufu nchini humo ikiwamo staa wa mitandao ya kijamii Dance General.

Leave your comment

Top stories