Angel Nyigu Akerwa na Wasanii Wasiounga Mkono Wasakataji Densi

[Picha: Angel Nyigu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msakataji densi maarufu kutoka Tanzania Angel Nyigu, ambaye anafahamika kwa ukaribu wake na Diamond Platnumz, ameelezea kukerwa na visa vya wanamuziki kutowaunga mkono wachezaji ambao wanahusika katika ngoma zao.

Soma Pia: Shilole Ajibu Madai Kuwa Alihudhuria Usikilizaji wa Albamu ya Alikiba Bila Mualiko

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa kijamii, Angel Nyigu alieleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuwaona wasanii wanachapisha video ya 'madancer' bila ya kushawishi wafuasi wao kuwaunga mkono wasakataji densi hao.

Kwa mujibu wa Angel Nyigu, 'dancers' pia huwekeza muda wao katika kuhakikisha kuwa kazi wanayofanya inachangia katika mafanikio ya muziki. Aliendelea kwa kuashiria kuwa kunafaa kuwe na kutegemeana baina ya wanamuziki na wachezaji.

"Kusema ukweli na kerwa na tabia za wasanii wanao post ma dancer wamecheza nyimbo zao halafu hawawatag hawa vijana wanahitaji kujulikana kwa kusupport mziki wenu show us support pia," ujumbe wa Angel Nyigu ulisomeka mtandaoni.

Soma Pia: Nyimbo Tano Bora za Hip-hop Kutokea Bongo Zinazogusia Suala la Pesa

 Angel Nyigu alipata uungaji mkono mwingi sana kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Miongoni mwa waliojitokeza na kumuunga mkono ni mwanamuziki nyota Barnaba Classic ambaye alisema ni jambo muhimu 'dancers' kutambuliwa kwa juhudi na mchango wao kwenye tasnia ya muziki.

"Fact because credibility it’s very important," Barnaba Classic aliandika maoni yake.

Angeli Nyigu ni miongoni mwa wachezaji ambao wamepata mafanikio makubwa sana na kufanya kazi na wasanii tajika kutoka Tanzania kama vile Zuchu na Diamond Platnumz. Angel pia amegonga vichwa vya habari baada ya kupata utezui kwenye tuza za AEAUSA katika kitengo cha 'Best Dancer/Group'.

Leave your comment

Top stories