Shilole Ajibu Madai Kuwa Alihudhuria Usikilizaji wa Albamu ya Alikiba Bila Mualiko

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka Tanzania Shilole amedai kuwa amehisi kukosewa na maneno ya mwanamuziki nyota Alikiba.

Alikiba hivi karibuni alidai kuwa hakumualika Shilole katika hafla ya usikilizaji wa albamu yake ya 'Only One King'. Kauli ya Alikiba iliibua maswali kuhusu vipi Shilole alikuwepo kwenye hafla hiyo bila mualiko.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Shilole Aachia Wimbo Mpya ‘Amsha Popo’

Hafla hiyo ilihudhuria na watu walioalikwa pekee. Shilole hatimaye amefungka kuhusu kauli ya Alikiba na tuhuma za yeye kuhudhuria hafla ya usikilizaji wa albamu ya 'Only One King' bila mualiko.

Katika taarifa aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Shilole alidai kuwa alihisi kukosewa mno na maneno ya Alikiba. Kwa mujibu wa Shilole, alipokea mualiko kutoka kwa Alikiba na hata mualiko huo ulichapishwa katika ukurasa wa kijamii wa Alikiba.

Soma Pia: Wasanii 5 Waliotazamwa Zaidi YouTube Tanzania Mwezi Oktoba, 2021

Aliongeza kuwa mara kwa mara yeye hukosewa lakini amechoka na hangebaki kimya tena.

''Hapana jamani, kila siku nakosewa nikitaka kuongea washauri wangu wanasema nikae kimya. Hili nimekosewa sana na siwezi kukaa kimya sasa mnanionea,'' Shilole aliandika mtandaoni.

Shilole aliendelea kwa kueleza kuwa Alikiba hajajipanga kulingana na ukubwa wake kama msanii. Alisema kuwa huenda Alikiba akakosa kujua mambo yanayoendelea katika timu yake na labda hili ndilo lililosababisha mkanganyiko huo.

''Umethibitisha kwamba wewe hauko ‘organized’. Kwa sababu, utasema nilipostiwa kwenye page yako na kutafutwa na watu wako wakati hawajakutaarifu. Kwa hiyo kwa ukubwa tunaotangaziwa unao Bwana Ali, unataka kusema hujui hata kilichopostiwa kwenye page yako rasmi katika siku yako muhimu?'' chapisho la Shilole lilisomeka.

Leave your comment