Nyimbo Mpya: Shilole Aachia Wimbo Mpya ‘Amsha Popo’

[Picha: Shilole Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Shilole ameachia wimbo mpya kwa jina la ‘Amsha Popo’.

Wimbo wa ‘Amsho Popo’ ni wa burudani na lengo lake kuu ni kuwafurahisha mashabiki kupitia densi. Kupitia mistari ya wimbo huo, Shilole pia anasimulia hali ya maisha yake na kujisifia kwa uwezo wake kimuziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny ‘New Chui’ EP, Alikiba ‘Bwana Mdogo’ na Ngoma Zingine Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii 

"Wanasema maneno, wala sijali, vidomo vidomo, wapishe mbali, Shishi masho popo... Shishi mashine, eeeh, kama mumekosa kazi shika jembe mkalime, usilete ubazazi, washa kiki niizime, Shishi ndio hufunga kazi, hakuna mwingine, kama unywele ninao, kama mkia ninao, kabeb fesi ninako, Shishi mama lao, kama mkwanja ninao, mkia ninao, kama mkia ninao, Shishi mama lao," Shishi anaimba kwenye ‘Amsha Popo’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Video ya ‘Bwana Mdogo’ Akimshirikisha Patoranking

Mdundo wa ngoma hii ni wa kasi na hivyo basi inakuwa ngoma nzuri ya kusakata densi nayo. Wimbo huo umetolewa kwa mfumo wa audio tu na hauna video. Mashabiki wanatarajia kuwa Shilole ataachia video ya ngoma hiyo hivi karibuni, japo msanii huyo bado hajazungumzia suala la utengenezaji wa video ya ‘Amsha Popo’.

Ngoma ya ‘Amsha Popo’ imepokelewa vyema na mashabiki na tayari ishapata maelfu ya watazamaji kwenye mtandao wa YouTube ndani ya muda mfupi wa uchapishaji wake. Shilole ni mmoja wa wasanii wa kike ambao wanafanya vizuri kwenye tasnia ya muziki ya Tanzania. Msanii huyo anajivunia ufuasi mkubwa katika mitandao tofauti ya kijamii.

Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Shilole ameachia wimbo mpya kwa jina la ‘Amsha Popo’.

Wimbo wa ‘Amsho Popo’ ni wa burudani na lengo lake kuu ni kuwafurahisha mashabiki kupitia densi. Kupitia mistari ya wimbo huo, Shilole pia anasimulia hali ya maisha yake na kujisifia kwa uwezo wake kimuziki.

"Wanasema maneno, wala sijali, vidomo vidomo, wapishe mbali, Shishi masho popo... Shishi mashine, eeeh, kama mumekosa kazi shika jembe mkalime, usilete ubazazi, washa kiki niizime, Shishi ndio hufunga kazi, hakuna mwingine, kama unywele ninao, kama mkia ninao, kabeb fesi ninako, Shishi mama lao, kama mkwanja ninao, mkia ninao, kama mkia ninao, Shishi mama lao," Shishi anaimba kwenye ‘Amsha Popo’.

Mdundo wa ngoma hii ni wa kasi na hivyo basi inakuwa ngoma nzuri ya kusakata densi nayo. Wimbo huo umetolewa kwa mfumo wa audio tu na hauna video. Mashabiki wanatarajia kuwa Shilole ataachia video ya ngoma hiyo hivi karibuni, japo msanii huyo bado hajazungumzia suala la utengenezaji wa video ya ‘Amsha Popo’.

Ngoma ya ‘Amsha Popo’ imepokelewa vyema na mashabiki na tayari ishapata maelfu ya watazamaji kwenye mtandao wa YouTube ndani ya muda mfupi wa uchapishaji wake. Shilole ni mmoja wa wasanii wa kike ambao wanafanya vizuri kwenye tasnia ya muziki ya Tanzania. Msanii huyo anajivunia ufuasi mkubwa katika mitandao tofauti ya kijamii.

https://www.youtube.com/watch?v=XqQKyV_y2N4

Leave your comment