Maua Sama Azungumzia Uhusiano Wake Na Nandy

[Picha: Maua Sama Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Maua Sama hivi karibuni ameongea hadharani kuhusu ukaribu alionao na mwanamuziki Nandy.

Nandy na Maua Sama ni wasanii wa kike wanaofanya vizuri sana nchini Tanzania. Pamoja na wote kuwa wasanii wakubwa, mara nyingi hawaonekani kuwa pamoja na hivyo kuzua tetesi miongoni mwa wadau wa muziki kuwa huenda wasanii hao hawana maelewano mazuri.

Soma Pia: Maua Sama Ataja Changamoto Alizopitia Katika Kuandaa Video ya ‘Zai’

Akiongea kwenye mahojiano ya hivi karibuni, Maua Sama alisema kuwa yeye na Nandy sio marafiki wa karibu sana lakini hiyo haimaanishi kwamba wana ugomvi au kuna mtafaruku kati yao.

Aliongeza kwamba yeye ni shabiki mkubwa sana wa kazi za Nandy.

"Kusema ukweli sijawasiliana nae muda lakini ni mtu ambae hatuna matatizo nina imani sina tatizo nae na yeye nadhani hana tatizo na mimi. At the same time mimi nakubali kazi zake sana na pia napenda harakati zake," alizungumza Maua Sama.

Kabla ya kuwa wasanii wakubwa Maua Sama na Nandy wote wawili walikuwa chini ya Tanzania House Of Talent (THT) ambayo ni shule ya kupika vipaji nchini Tanzania.

Soma Pia: Maua Sama Azungumzia Collabo yake na T Pain, Aeleza Sababu Hajaachia Kazi Hio Bado

Maua Sama alizidi kueleza kuwa hapo zamani walikuwa na ukaribu kwa sababu walikuwa wanakutana lakini sasa hivi kila mtu yuko kivyake na ndio maana hawaonekani pamoja.

"Kila mtu sasa hivi anafanya mambo yake yale tuliyofundishwa pale (THT) kila mtu anayaimplement kwa njia yake kwa hiyo hakuna haja ya kusema tutafutane kama hakuna urafiki huo ule wa kushibana," alizungumza Maua Sama.

Kwa sasa Maua Sama anatamba na ngoma yake ya ‘Zai’ huku mashabiki wana hamu sana ya kusikia ngoma yake na T Pain.

Leave your comment