Maua Sama Ataja Changamoto Alizopitia Katika Kuandaa Video ya ‘Zai’

[Picha: Tuko]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika nchini Tanzania Maua Sama amefunguka kuhusu changamoto alizopitia wakati anaandaa kanda ya ngoma yake ya ‘Zai’ ambayo aliiachia siku ya jana.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni kwenye XXL ya Clouds FM, Maua Sama ameeleza kuwa alitumia takribani siku tatu kuweza kukamilisha video ya ‘Zai’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Maua Sama Aachia Video ya ‘Zai’

 Kulingana na Maua Sama, vdeo hio ilichukua siku tatu kwa kuwa hakupenda mhusika wa kwanza ambaye alichaguliwa kucheza nafasi ya Zai kwenye video hiyo, hivyo akaomba aletwe mwingine.

"Tulishoot kwa siku tatu, the first day mvua ilinyesha, the second day hakika hakuwepo alafu pia Zai nililetewa sikumpenda hivyo ikabidi tutafute mwingine it was hard to find a right perfect girl ambaye ataweza akafit kwenye video," alisema Maua Sama.

Hata hivyo, Maua alitanabaisha kuwa ilipofika siku ya tatu, ndipo waliweza kumpata Hakika Reuben na ndio siku hiyo ambapo waliweza kufanya video hiyo, ambayo tangu kuachiwa kwake imeleta gumzo kutokana na ubunifu pamoja uhalisia uliopo.

Soma Pia: Maua Sama Azungumzia Collabo yake na T Pain, Aeleza Sababu Hajaachia Kazi Hio Bado

Maua Sama pia alitumia mahojiano hayo kutoa shukrani zake kwa rapa kutokea kundi la Weusi Joh Makini, ambaye alitumia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliweka video ya ngoma hiyo akimsifia Maua Sama kwa kuweza kuimba vizuri, na kufanya Bongo Fleva safi.

 "Joh Makini ni brother na kama yeye ameona na kusema kuhusu ngoma ya Zai kama naurudisha muziki wa Bongo Fleva cause wadau wanadai kuna muda kidogo Bongo Fleva kama inapoteza direction. Ile post ya Joh ina maana kubwa sana kwangu I really appreciate," alizungumza fundi huyo wa RnB kwa hapa nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=MAmFhxxGJoc

Leave your comment