Nyimbo Mpya: Maua Sama Aachia Video ya ‘Zai’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Maua Sama ameachia rasmi video ya ngoma yake ya ‘Zai’ ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa muziki.

Kwenye video hii ya ‘Zai’, Maua Sama amevaa uhusika wa mwanadada ambaye anamsihi binti aitwaye ‘Zai’ aache tabia ya kutoka kimapenzi na mpenzi wake.

Soma Pia: Maua Sama Azungumzia Collabo yake na T Pain, Aeleza Sababu Hajaachia Kazi Hio Bado

Ili kunogesha zaidi video hii, Maua Sama amefanya video hii kwenye maeneo ya uswahilini au mtaani ili kuleta zaidi uhalisia.

Kilichovutia zaidi kwenye video hii ni kushirikishwa kwa Hakika Ruben ambaye ni mmojawapo ya wachekeshaji wakubwa nchini Tanzania. Reben ameshirikishwa kama mpenzi wa Maua Sama, kitu ambacho kimevuta sana hisia za mashabiki.

Video hii imetayarishwa na Director 5 ambaye amehusika kutengeneza video za wanamuziki tofauti tofauti kama Jux, Rayvanny, Johmaker na Mac Voice kutokea Next Level Music.

Kufikia sasa, video hii ya ‘Zai’ imeshatazamwa mara arobaini elfu kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Maua Sama Afunguka Kuhusu Tatizo la Kiafya Lilioathiri Utendakazi Wake Kimuziki

Hii ni video ya pili ya Maua Sama kwa mwaka huu, ya kwanza ikiwa ni video ya ‘Wivu’ aliyomshirikisha Aslay.

Baada ya video hii, mashabiki wanasubiri kwa hamu sana video ya ‘Away’; ngoma ambayo ameshirikiana na Young Lunya.

https://www.youtube.com/watch?v=MAmFhxxGJoc

Leave your comment