Maua Sama Azungumzia Collabo yake na T Pain, Aeleza Sababu Hajaachia Kazi Hio Bado

[Picha: Maua Sama Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutokea Tanzania Maua Sama hatimaye amethibitisha kuwa collabo yake na rapa T Pain kutokea Marekani ipo njiani.

Wiki iliyopita, Maua Sama kupitia akaunti yake ya Instagram alionesha mazungumzo yake na rapa T Pain, iliyoashiria kuwa wako jikoni kuandaa collabo baina yao.

Soma Pia: Wasifu wa Maua Sama, Nyimbo zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

Akizungumza kwenye redio moja hapa nchini Tanzania, Maua Sama amesema kuwa wimbo huo upo ila tu kuna masuala katika maandalizi ya video bado hajayakamilishwa.

"Collabo na T Pain inakuja ni mimi tu ambaye najichelewesha kwenye video ila this Friday mpaka November anything can happen. You need to stay close to me. Very very close to me," alitanabaisha Maua Sama.

Aidha, Maua Sama aliwashukuru mashabiki kupokea vizuri ngoma zake mbili alizozitoa hivi karibuni yaani ‘Away’ aliyomshirikisha Young Lunya na ‘Zai’.

Soma Pia: Maua Sama Afunguka Kuhusu Tatizo la Kiafya Lilioathiri Utendakazi Wake Kimuziki 

Msanii huyo pia amedokeza kuwa huenda akaendelea na utamaduni wake wa kutoa ngoma mpya kila ijumaa saa mbili na nusu asubuhi.

"Thank you so much for your support Mashabiki zangu wananifanya niendelee na mpango wangu wa Sama Friday, yaani kila ijumaa saa mbili na nusu asubui ni moto tu yaani stay tuned this Friday," alizungumza Maua Sama.

Kinachosubiriwa kwa sasa kutoka kwa Maua Sama ni video za ‘Away’ na ‘Zai’ ambazo huenda zikaingia sokoni hivi karibuni.

Leave your comment