Wasifu wa Maua Sama, Nyimbo zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Maua Sama ni nani na ana miaka ngapi?

Jina la usanii: Maua Sama

Tarehe ya Kuzaliwa: 27 Agosti 1990

Aina ya Muziki: Bongo Fleva

Thamani Yake: Haijulikani kwa sasa

Maua Sama alizaliwa nchini Tanzania mnamo tarehe 27 Agosti 1990. Alianza kuimba akiwa mdogo sana. Wazazi wake walimtaka azingatie masomo yake badala ya muziki.

Maua Sama alianzaje muziki na lini?

Maua Sama aligunduliwa kwa mara ya kwanza na Mwana FA mnamo 2013 baada ya kusikiliza nyimbo zake kadhaa. Mwana FA alimleta Dar es Salaam na pamoja wakashirikiana kwenye miradi kadhaa.

Miongoni mwa nyimbo zake za kwanza kuachia ni 'Mahaba Niue' ambayo alitoa mwaka wa 2017.Toka hapo, ameendelea kutoa vibao zaidi kwa sauti yake nzuri na ya kupendeza. Mnamo 2018, aliachia ‘Iokote’ aliyomshirikisha msanii wa bongo Hanstone. Wimbo huu ulimpa umaarufu mkubwa sana kwa njia ambayo hakutarajia. Hii ilimweka kati ya majina kubwa katika tasnia ya muziki ya Tanzania. Amefanya ushirikiano na watu wengine wakubwa nchini Tanzania kama vile Harmonize na Vanessa Mdee.

Je Maua Sama ana albamu ngapi?

Maua Sama hana albamu yoyote, lakini anatarajiwa kuachia albamu na EP ndani ya mwaka huu. Humo ndani atawashirikisha wasanii mbali mbali.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

Nyimbo zake Bora ni gani?

  • Iokote
  • Wivu
  • Niteke
  • Can Dance
  • Amen
  • This love
  • Katu Katu

Maua Sama anachumbiana na nani?

Maua Sama hajaweka hali halisi kuhusu mahusiano yake.

Leave your comment