Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Katika mziki wa Bongo ubabe wa wasanii unaendelea kushindaniwa kila kukicha. Katika nakala hi,  tunaangazia nyimbo tano zinazovuma wiki hii kutoka Bongo.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Kelebe - Rayvanny ft Innoss’B

Huu ndio wimbo ulioachiwa wikendi iliyopita na Rayvanny akimshirikisha msanii gwiji kutoka Congo Innoss’B. Kwa sasa, ‘Kelebe’ imechukua nafasi ya kwanza kwenye trends na watazamaji zaidi ya million moja Nukta nane kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Konde Music Worldwide Kuachia Albamu Nne Mwaka wa 2021

https://www.youtube.com/watch?v=V7sBxHz_nHE

Nobody - Anjella

Hii ni kazi yake Anjella kutoka Konde Gang iliyopokelewa kwa ukubwa sana. ‘Nobody’ ni wimbo wa mapenzi na kufikia sasa una watazamaji zaidi ya milioni mbili kwneye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=-NCqC_BoUXc

Attitude - Harmonize ft Awilo Longomba and H baba

Ndani ya wiki tatu, wimbo ‘Attitude’ wa Harmonize umefikisha watazamaji zaidi ya million tisa nukta nane kwenye YouTube. Katika wimbo huu,Harmonize aliwashirikisha wasanii Awilo Longomba na H-baba.

https://www.youtube.com/watch?v=bElhxzQweYQ

Yes - Mbosso ft Spice Diana

Huu ni wimbo wa kumuomba mchumba kuwa mke wa mtu au tuseme harusi. Kwa sasa wimbo huu unashikilia nambari nne YouTube na watazamaji zaidi ya milioni mbili nukta nne.

https://www.youtube.com/watch?v=NClIIN8FgF4

Komesha – Lava lava

‘Komesha’ ni wimbo mpya kutoka kwa msanii Lava Lava. Katika ngoma hii, Lava Lava anapigania penzi lake. Kufikia sasa, ‘Komesha’  ina watazamaji zaidi ya laki nani.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Video Mpya ‘Komesha’

https://www.youtube.com/watch?v=XmT_CsFAtqc

Leave your comment