Konde Music Worldwide Kuachia Albamu Nne Mwaka wa 2021

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi Mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ametangaza kuwa kambi hio itaachia albamu nne mwaka huu wa 2021.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Kupitia Instastories kwenye ukurasa wake, Harmonize alidokeza kuwa albamu za wasanii wake Killy, Cheed, Anjella, Ibraah na yeye mwenyewe zipo tayari.

“Killy Album Done! Cheed Album Done! Anjella Album Done! Sasa mie #Highshool si itachelewa….Hapo Chinga Kaambiwe atie mawe matatu ya moto kwanza ila albamu kashakamirisha….”aliandika Harmonize.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Sukari na Video Zingine Bora za Zuchu Zinazovuma Bongo

Vile vile ametaja kuwa huu ni mwaka wake wa kung’aa kimziki.  Kwa wiki mbili sasa, Harmonize amepiga kambi nchini Nigeria kukamilisha maandalizi ya albamu yake ya ‘High school’.

Katika ziara zake, Harmonize aligundua kuwa mziki wa bongo hauna ukubwa nchini Nigeria

Harmonize aliongezea kuwa mziki wa Afrika Kusini Amapiano umekita mizizi barani Afrika huku akitumai kuwa mziki wa Singeli kutoka Tanzania utapata umaarufu huo hivi karibuni.

Soma Pia: Muziki wa Singeli Tanzania: Kwa Nini Singeli Haitambi Kama Bongo Fleva?

“South Africa is a champion for now African Music ipo mikononi mwao….Sound Yao imeshika kila sehemu . I see Singeli Next, take it from me. Ifiche itawasaidia kama kumbukumbu…” aliandika Harmonize.

Hivi karibuni katika chati za YouTube Harmonize amempiku Diamond Platnumz na kuwa msanii wa pili baada ya Mbosso kwa wasanii wanaovuma Bongo sana mwezi huu wa Mei.

 

Leave your comment