Muziki wa Singeli Tanzania: Kwa Nini Singeli Haitambi Kama Bongo Fleva?
4 May 2021
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Muziki wa Singeli unaendelea kubobea nchini Tanzania kila kukicha ila wasanii wanaojulikana kwa Singeli hawajapewa kipaumbele kama wale wa Bongo Fleva. Katika nakala hii, tunaangazia sababu tunazodhania zinafanya mziki huo Kuwa chini .
Pata Ubashiri wa Mechi Kati ya Real Madrid na Chelsea
Ubabe wa Bongo Fleva
Mziki wa Bongo Flava kwa sasa ndio fani kubwa sana nchini Tanzania na pia ndani ya Afrika Mashariki. Hivyo mziki huo umefanya singeli kufifia na kutopata kipaumbele kwa mashabiki na hata wasani wengine kususia mziki huo.
Pakua Nyimbo Zake Meja Kunta Bure Kwenye Mdundo
Wasanii wa Singeli sio Maarufu Sana
Wasanii wa mziki wa Singeli sio maarafu kama wale wa Bongo Fleva. Ni wasanii wachache wanaotambulika kama vile Dulla Makabila, Meja Kunta na Balaa Mc . Hawa ndio wamechukua kipaumbele kupigania mziki huo.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo
Ukosefu wa msaada kutoka kwa wasanii wakubwa
Hivi karibuni tumeona wasanii wa Singeli wakihusishwa na wasanii wenzao wa bongo Flava, ila si wote wanapata usaidizi huo. Kwa sasa ili kunadhifisha hadhi ya mziki wa Singeli wasanii tajika wanafaa kuwashika wengine wa Singeli mkono.
Uendelezaji na Uuzaji
Katika nyakati hizi za kidijitali sio tu vituo vya habari vimetenga sana wasanii wa mziki wa Singeli haswa katika kucheza mziki huo. Wachache tu ndio hupata fursa hiyo na hata kuwa n mahojiano na wasanii wa mziki wa Singeli.
Lugha Tumika
Mfumo wa mziki wa Singeli hutumia lugha ya Kiswahili pekee wakati mziki wa Bongo Fleva ya sasa huchanya ndimi za Kiswahili na Kiingereza ili kufikia soko zote, Singeli ni mziki halisi wa Bongo na mabadiliko ya lugha inaweza kuwa hatari kwa mdundo huo. Hivyo basi mziki wa Singeli utaendelea kuwa na hadhira inayokielewa Kiswahili tu ama lugha za Kitanzania tu. Hii pia ni chanagamoto kwani mziki huo utakuwa na mashabiki nchini Tanzania nan chi zingine zinaoelewa Swahili pekee.
Leave your comment