Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwaka 2021 umeanza kwa kishindo kwa msanii Nandy. Nandy ameweza kuachia mziki mzuri kwa kasi chini ya miezi mitatu ikiwemo EP yake ya mziki wa injili ‘Wanibariki’. Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo hizo alizoachia Nandy:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ‘Leo Leo’ Akimshirikisha Koffi Olomide

Leo Leo ft Koffi Olomide

Ni wimbo unaoafikiana ana maudhui ya mapenzi. Hii ndio kazi kubwa zaidi yake Nandy mwaka na amemshirikisha msanii mkongwe wa mziki wa Lingala Koffi Olomide. Kufikia sasa, kanda ya wimbo huu ina watazamaji zaidi ya milioni moja nukta sita.

https://www.youtube.com/watch?v=_8rFTFKMjNU

Number One

Huu ni wimbo mzuri ambapo wapenzi wawili wanaelezea hamu na mapenzi yao kwa kila mwingine. Kweny wimbo huu, Nandy amemshirikisha JoeBoy kutoka Nigeria. Kufikia sasa, wimbo huu una watazamaji zaidi ya millioni mbili nukta tano.

https://www.youtube.com/watch?v=8fO1swbTvQk

Wanibariki

Huu ni wimbo ambao Nandy anaangazia safari yake ya maisha na kumshukuru Mungu kwa baraka alizomjalia. Anaimba na kusema ni Mungu tu amefanya hatetemeki.

https://www.youtube.com/watch?v=O66DTwFGAlI

Umenifaa

Huu ni wimbo unaoelezea namna Mungu amekua mtetezi katika maisha yake. Anaelezea jinsi mambo ya dunia yamekua mazito ila Mungu alijionyesha na kumsaidia haswa katika wakati wa shida.

https://www.youtube.com/watch?v=kiImAcRM_h4

Nipo Naye

Huu ni wimbo wa maombi ya mwanamke anayemshukuru Mungu kwa kuwa sehemu ya maisha yake kila wakati. Kwa kutomkatia tamaa kwa sababu ya njia zake za dhambi, anamsifu Mungu kwa kumpa kila wakati nafasi nyingine ya maisha.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia EP Mpya ‘Wanibariki’ Yenye Mziki wa Injili

Leave your comment