Nyimbo Mpya: Lava Lava Aachia Video Mpya ‘Komesha’

[Picha: Lava Lava Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Lava Lava ameachia video ya wimbo wake ‘Komesha’. Hii ni video ya pili kutoka EP yake ya ‘Promise’ alioachia rasmi mwezi Februari kuadhimisha siku ya wapendanao.

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

‘Komesha’ ni wimbo wa mapenzi ambapo Lava Lava anamuimbia binti mmoja ambaye amempagawisha kwa urembo wake.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Anaeleza urembo wake kutumia maneno matamu huku akimuonya kutoskiliza watu wanaosema yeye si muwaminifu katika uhusiano na kumuomba acheze bila kujizuia.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Sukari na Video Zingine Bora za Zuchu Zinazovuma Bongo

“Sitojifanya maproso, Nikaja kukudanganya, Ukakumbuka before,Ntakupenda mpaka useme poo Kwako nitang'ang'ana I'll never let you go…” aliimba Lava Lava.

Anadai kuwa atampenda binti yule hadi achoke naye ila kwa sasa yuko tayari. Kanda hii ina picha za kuvutia kuanzia kwa kina dada warembo na kaka wenye uzuri wao.

Soma Pia: Muziki wa Singeli Tanzania: Kwa Nini Singeli Haitambi Kama Bongo Fleva?

Kinachojitokeza wazi kwenye wimbo huu ni ushahiri wa Lava lava katika uandishi wa mistari yake. 

Kanda hii ilifanyiwa maandalizi na director Hascana. Kwa sasa wimbo huu umepokelewa vizuri na mashabiki huku kwenye mtandao wa YouTube akipata watazamaji zaidi ya laki moja.

Soma Pia: Wasifu wa Vanessa Mdee, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Kazi hii inakua kazi yake mpya zaidi huku akitarajiwa kuachia albamu yake mwaka huu pamoja na wasanii wengine nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=XmT_CsFAtqc

Leave your comment