Maua Sama Afunguka Kuhusu Tatizo la Kiafya Lilioathiri Utendakazi Wake Kimuziki

[Picha: Maua Sama Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki kutoka Tanzania Maua Sama hatimaye amefunguka kuhusu sababu iliyomfanya kuwa kimya kwenye muziki kwa muda wa takriban miezi saba.

Maua Sama hajaachia wimbo wowote tangu wimbo wake wa 'Wivu' aliyomshirikisha msanii Aslay. Ukimya wa Maua Sama uliibua hisia tofauti mtandaoni huku wengi wakijiuliza ni nini kilichotokea hadi malikia huyo wa bongo kunyamaza.

Soma Pia: Babu Tale Aguswa na EP Mpya ya Mwasiti ‘The Black Butterfly’

Hatimaye, Maua Sama amefunguka na kufichua kuwa alilazimika kuwa kimya kwa sababu ya tatizo la kiafya alilokuwa nalo.

Aliweka wazi kuwa ameugua tatizo la kutoweza kusikia vizuri na pia matatizo mengine yaliyoathiri kinywa chake. Matatizo haya ya kiafya yalifanya iwe ngumu Maua Sama kufanya shughuli zake za kimuziki haswaa kuimba na hivyo basi kuiathiri taaluma yake ya muziki.

 Maua Sama hata hivyo ametangaza kurudi kwake baada ya kupona. Alimshukuru Mungu kwa hilo na kuwaahidi mashabiki wake burudani.

"Hey lovers, Mungu wetu mwema sana. Tatizo langu la kupoteza uwezo wa kusikia vizuri (tinittus) kwa zaidi ya miezi 7 na matatizo ya kinywa sasa yamepona. Mungu mwema. Kile kitu nakuja kuwafanya chiii. Vocal most wanted. I can't wait," chapisho lake Maua Sama mtandaoni lilisomeka.

Soma Pia: Zuchu Ajibu Madai ya Kutumia Ushirikina Ili Kupata Mafanikio Kwenye Muziki

Kwa sasa, macho yote yako kwake Maua Sama ambaye ako na kazi kubwa ya kurudi tena kwenye tasnia ya muziki na kuendelea pale ambapo aliwachia.

Maua Sama ni mmoja wa wasanii wa kike wanaofanya vizuri sana Afrika Mashariki na wenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni.

Leave your comment