Zuchu Ajibu Madai ya Kutumia Ushirikina Ili Kupata Mafanikio Kwenye Muziki

[Picha: Wasafi TV Facebook]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Zuhura Othman Soud, ambaye anafahamika kwa jina la kisanii kama Zuchu amekanusha na kutupilia mbali madai yanayohusisha mafanikio yake ya kimuziki na ushirikina.

Soma Pia: Zuchu Amsifia Nandy, Adokeza Kuwa Hana Tatizo Kufanya Kolabo Naye

Akizungumza wakati anahojiwa Wasafi TV, Zuchu alikanusha tuhuma hizo na kuongezea kuwa hajawahi jihusisha na ushirikina wa aina yoyote. Alisistiza kuwa yeye kibinafsi hawezi amini nguvu za mwanadamu mwenzake na hajawahi enda kwa mganga.

Zuchu alitetea mafanikio yake kwa kusema kuwa yanatokana na bidii yake kimuziki na kwa Mungu.

“Sijawahi Kwenda kwa mganga, Siwezi kuamini nguvu za mwanadamu mwenzangu, Mafanikio yangu ni kutokana na Mwenyezi Mungu na sijawahi kufanya ushirikina,” Zuchu alisema katika mahojiano kwenye kipindi cha Big Sunday Live.

Zuchu amesifiwa sana na wadau wengi kutokana na mafanikio yake kwenye tasnia ya muziki ndani ya muda mfupi sana.

Soma Pia: Jay Melody Azungumzia Ripoti Kuwa Amejiunga na Lebo ya Rayvanny Next Level Music

Kufikia sasa imepita mwaka mmoja na miezi mitano tangu Zuchu kutambulishwa kama mwanachama wa lebo ya WCB. Ngoma anazotoa Zuchu huvuma mtandaoni na kutazamwa na mamilioni ya mashabiki, si Tanzania tu bali pia nje ya Tanzania.

Mojawapo ya tukio lililovutia wengi sana na kuacha alama nzuri katika taaluma ya Zuchu mwaka huu ni tamasha lake la Zuchu Homecoming. Tamasha hilo ambalo lilikuwa la kwanza kwa Zuchu kama msanii lilipata mafanikio makubwa na kuhudhuriwa na watu wengi sana.

Zuchu pia amedokeza kuwa kutokana na mafanikio hayo, ataanda tamasha lingine.

Leave your comment