Zuchu Amsifia Nandy, Adokeza Kuwa Hana Tatizo Kufanya Kolabo Naye

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka lebo ya WCB Zuchu amemsifia msanii mwenzake Nandy kwa bidii yake katika muziki. Zuchu alisema kuwa Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike ambao kwa sasa wanavuma sana katika tasnia ya burudani ya Tanzania.

Zuchu alitoa kauli hiyo katika kipindi cha Big Sunday Live ambapo aliulizwa kuchagua msanii anayemkubali baina ya Nandy na Maua Sama.

Soma Pia: Nandy Amsifia Rais Samia Suluhu Kwa Kukuza Sanaa ya Muziki Tanzania

Ulikua uamuzi mgumu kwa Nandy kwani kwa maoni yake wasanii wote wanafanya vizuri sana ila mwishowe alimchagua Nandy. Zuchu aliongeza kuwa anapenda sauti ya Maua Sama na akampa pongezi kwa hilo.

"Shout out to Maua I love her voice, lakini I'll have to give it to Nandy. She's doing really good, so Nandy," Zuchu alisema.

Aidha, Zuchu aliashiria kuwa hana tatizo kufanya kazi na wasanii hao wawili na yeyote atakayemtafuta wafanye kazi pamoja basi atakubali.

Soma Pia: Nandy Atoa Shukrani Baada ya Tamasha lake Dar es Salaam Kupata Mafanikio Makubwa

Kilichowashangaza wengi hata hivyo ni kuwa Zuchu anamfuata Maua Sama kwenye mtandao wa Instagram ila hamfuati Nandy.

Tuhuma hata hivyo zimewahi ibuka mtandaoni kuashiria kuwa huenda kuna uhasama baina ya Nandy na Zuchu. Japo wasanii hao wawili hawajawahi kuwa na tofauti za kibanfsi, madai hayo yamewaandama.

Zuchu na Nandy ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao wanaheshimika barani Afrika kutokana na mafanikio yao kimuziki.

Leave your comment