Nandy Atoa Shukrani Baada ya Tamasha lake Dar es Salaam Kupata Mafanikio Makubwa

[Picha: AFRICAMM]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Nandy amejitokeza na kutoa shukrani baada ya Tamasha lake la Nandy Festival lililotua Dar es Salaam kupata mafanikio.

Nandy alitoa shukrani katika ujumbe aliouchapisha mtandaoni. Katika chapisho hilo, Nandy alikiri kuwa safari ya tamasha la Nandy Festival ambalo limekua katika mikoa tofauti haijakuwa rahisi.

Read Also: Joel Lwaga aweka wazi jina la EP yake

Ila alimshukuru Mungu pamoja na mashabiki wake kwa kumuunga mkono katika kuandikisha rekodi mpya katika taaluma yake ya usanii. Nandy pia alipeleka shukrani zake kwa wadau mbali mbali kama vile wasanii, wanahabari na makampuni yaliohusika katika njia moja au nyingine kufanikisha tamasha lake.

Read Also: Tunda Man Amkosoa Chidi Benz Baada Ya Kuzungumziaa Uhusiano Wake Na Diamond

"Haikuwa rahisi kuianza hii safari na kuimaliza salama ni mkono wa Mungu na support ya mashabiki zangu mmeweka historia ndani ya moyo wangu na legacy isiyo futika! Asanteni sana sitoacha kushukuru. Bila kusahau makampuni yote yaliyo ungana na mimi kufanikisha hili mmetisha sana. Bila kusahau media na blogs zote kwa kushirikiana na mimi barabaraaa kupeleka habari kuwa nandy festival iko nchini. Wasanii wenzangu sina cha kuongea u guys your amaizing nawashukuru sana. Thank you for Nandy festival 2021," chapisho la Nandy mtandaoni lilisomeka.

Chapisho la Nandy aidha liliashiria kuwa tamasha la Nandy Festival huenda imekamilika kwa mwaka huu. Nandy amepata mafanikio makubwa sana kutokana na tamasha zake ambazo pia zilimwezesha kuleta wasanii wakubwa nchini Tanzania.

Mmoja wa wasanii wakubwa sana barani Afrika ambaye aliweza kutumbuiza katika Nandy Festival mwaka huu ni JoeBoy kutoka Nigeria.

Leave your comment