Joel Lwaga aweka wazi jina la EP yake

[Picha: Joel Lwaga Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Injili anayefanya vizuri kwa sasa nchini Tanzania Joel Lwaga ameanika jina la EP yake mpya ambayo itaitwa "Trust".

Tunda Man Afunguka Kuhusu Marafiki Wake Kumshusha Kimuziki

Joel Lwaga ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo sambamba na jina hilo ametangaza kuwa EP hiyo itaachiwa Septemba 10 ya mwaka huu na ameandika "Good news ijumaa ijayo tarehe 10 September tutapata baraka ya nyimbo tano kwa mpigo katika platform zote" EP ya "Trust" haitashirikisha msanii yeyote ila badala yake nyimbo zote tano zinafuma EP hiyo zitafanywa na Lwaga peke yake na nyimbo hizo ni "Mifupani", "Specialist", "Nivushe", "Nitakuamini" na "Ogadoh".

Kwenye ukurasa wake wa Instagram pia Joel Lwaga ameeleza kwanini ametoa Trust EP na ameandika "Kuna wakati kuamini huwa rahisi na kuna wakati kuamini huwa ai rahisi wakati ambapo si rahisi hapo ndipo kuamini halisi"

Ikumbukwe kuwa Joel Lwaga alitoa EP yake ya "Unaweza" Juni 2019 na EP hiyo ilisheheni nyimbo tano ikiwemo "Sitabaki Kama Nilivyo" wimbo uliofanya vizuri sana hapa nchini Tanzania. Kwa nchini Tanzania wasanii wengi wameonekana kuwa na mwamko wa kutoa EP kwani kwa mwaka huu. Wasanii waliotoa EP kwa mwaka huu ni pamoja na Ibraah, Ice boy, Lavalava, Ziddy Value, Nandy na Mabantu.

Leave your comment