Tunda Man Afunguka Kuhusu Marafiki Wake Kumshusha Kimuziki

[Picha: Tundaman Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu wa bongo fleva Tunda Man amedai kuwa marafiki wake wa karibu walihusika pakubwa katika kumshusha kimuziki.

Tunda Man alikuwa msanii mwenye ushawishi mkubwa sana katika enzi za kale za bongo, ila kwa sasa nyota yake kidogo imefifia. Akizungumza na mwanahabari wa Wasafi TV, Tunda Man alisema kuwa amelazimika kuwadondosha baadhi ya marafiki wake wa karibu, kwani anaamini hawasaidii taaluma yake ya muziki.

Killy Aachia "Ni Wewe" Akimshirikisha Harmonize

Tunda Man hata hivyo alisistiza kuwa ni lazima mtu awe na marafiki katika maisha, ila cha muhimu ni kutambua kuwa wapo marafiki ambao watamfanya mwenzao kuyumba. Kikubwa ni kuwatambua marafiki hawa na kuwadondosha ili kuleta amani na maendeleo katika maisha yako. Kwa mujibu wa Tunda Man, amedondosha asilimia sabini ya marafiki wake haswaa wale aliokuwa na uhusiano wa kimuziki.

"Muziki wangu ume shake sana hapa katikati kwa sababu ya marafiki. Lazima uwe na marafiki, lakini kuna marafiki ambao ukiwa nao, lazima utayumba katika maisha. Na hakuna kitu kibaya kama snitch umfanye ndugu, hilo balaa. Kwa hivyo point kubwa mimi niliowafanya ndugu zangu ndio walionipotezea muziki wangu. This time nimepunguza asilimia sabini ya marafiki katika muziki wangu," Tunda Man alieleza. Kauli ya Tunda Man inatokea takriban wiki mbili baada ya yeye kuachia wimbo wa 'Mpunguze' unaozungumzia umuhimu wa kuwaondoa baadhi ya marafiki katika maisha haswaa wale bandia.

 

Leave your comment