Tunda Man Amkosoa Chidi Benz Baada Ya Kuzungumziaa Uhusiano Wake Na Diamond

[Picha: Tundaman Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika Chidi Benz hivi maajuzi aliibua hisia mtandaoni baada ya kudai kuwa mwanamuziki Tunda Man hana uhusiano mzuri na mwenzake Diamond.

Kauli hiyo ya Chidi Benz aliyoitoa katika mahojiano na Wasafi FM haijampendeza Tunda Man. Tunda Man amemkosoa Chidi Benz kwa kudai kuwa sio vizuri yeye kuzungumzia uhusiano wake na wasanii wengine haswaa kwa kugusia uhasama.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny na Harmonize Waongoza Wanamuziki wa Bongo Waliotazamwa Zaidi YouTube Mwezi Agosti

Alieleza kuwa yeye pia hawezi akazungumzia uhasama ambao Chidi Benz ako nao na wasanii wengine. Tunda Man hata hivyo licha ya kumkosoa Chidi Benz, alidai kuwa Chidi Benz ni kama ndugu yake na ako na mchango mkubwa katika taaluma yake ya muziki.

Chidi Benz na Tunda Man wamekuwa marafiki wa karibu tangu enzi za kale za bongo na hata washawahi kushirikiana katika wimbo wa 'Neilah'.

"Chidi Benz ni brother wangu, amefanya niwepo kwenye muziki. Chidi Benz amenitoa katika muziki, yaani watu wamenijua kwa sababu ya kupitia Chidi Benz. Kwa hiyo siwezi kusema chochote kibaya kwa ajili yake, namrespect na chochote anachokisema nakiheshimu. Lakini kunizungumzia kwamba mimi nina bifu na mtu sio kitu kizuri.

Maana hata yeye watu ambao ana bifu nao siwezi kuwazungumzia," Tunda Man alisema. Tunda Man alisisitiza kuwa tofauti na alivyosema Chidi Benz, yeye hana uhasama wala ubaya na Diamond Platnumz. Japo hawana ukaribu kama ilivyokuwa zamani, Tunda Man alisema pia hawana tofauti. 

Leave your comment