Jay Melody Azungumzia Ripoti Kuwa Amejiunga na Lebo ya Rayvanny Next Level Music

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Jay Melody kwa mara ya kwanza ameongelea kuhusu tetesi za yeye kuwa chini usimamizi wa Next Level Music ambayo ni lebo ya mwanamuziki Rayvanny.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na Lil Ommy, Jay Melody alisema kuwa hajaingia mkataba wowote na Rayvanny na wala hayuko chini ya Next Level Music.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu Kuu Iliyochelewesha Albamu Yake

"Mpaka sasa sijasainiwa sehemu yoyote sijajua plan za Rayvanny lakini mimi sina tatizo kwenye kusain kazi na mtu yeyote ambaye tunaendana nae," alizungumza Jay Melody.

Mtunzi huyo wa ngoma ya ‘Huba Hulu’ aliongezea kwa kusema "Biashara kubwa lakini pia itakuwa na faida kwake na kwangu pia (Rayvanny) hata ingekuwa sio Rayvanny ingekuwa mtu mwingine tungesain lakini mpaka sasa sijasaini nae."

Kauli hiyo kutoka kwa Jay Melody imeweza kutoa majibu ya sintofahamu iliyokuwepo kuhusu Jay Melody kusainiwa Next Level Music baada ya msanii huyo kuonekana kwenye makao makuu ya lebo hiyo wiki kadhaa nyuma akiwa studio.

Aidha, Jay Melody ameweka wazi kuwa licha hayupo kwenye lebo hiyo ya Next Level Music, alikuwa ni mojawapo ya watu wa kwanza kuambiwa kuwa Rayvanny anafungua lebo yake mwenyewe.

Soma Pia: Meja Kunta Atangaza Ujio wa EP Yake Mpya

"Kuna wakati aliniambia (Rayvanny) mi ntafungua lebo na kitu kama hicho. Mi nafkiri nilikuwa miongoni mwa watu wa mwanzoni kabisa kujua mchongo huo kabla haujawa viral lakini after hapo hakikutokea chochote," alizungumza Jay Melody.

Ikumbukwe kuwa wiki kadhaa nyuma, Jay Melody alidokeza kuwa yeye pamoja na Rayvanny wana ngoma ya pamoja ambayo ni ‘Huba Hulu’ remix lakini bado ipo kapuni.

Leave your comment