Babu Tale Aguswa na EP Mpya ya Mwasiti ‘The Black Butterfly’

[Picha: Mwanaspoti]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Walimwengu wanasema sikio siku zote halikatai muziki mzuri na dhana hiyo imeonekana dhahiri shahiri baada ya meneja wa msanii Diamond Platnumz Babu Tale kuonesha kuguswa na EP mpya ya mwanamuziki Mwasiti yenye jina ‘The Black Butterfly’.

Babu Tale ambaye pia ni muanzilishi wa chapa ya Tiptop Connection ameonesha furaha yake kuhusu EP hiyo ya Mwasiti kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kuandika: "Leo nimefurahi kuona baada ya muda mrefu mrembo mwenye sifa ya utulivu Mwasiti kaja na EP yake. Umeniguaa Mama."

Soma Pia: Zuchu Ajibu Madai ya Kutumia Ushirikina Ili Kupata Mafanikio Kwenye Muziki

Taarifa hiyo kutoka kwa Babu Tale ilipokelewa kwa shangwe sana na Mwasiti ambaye alionekana kumshukuru mkuu huyo kwa kumuunga mkono.

EP ya ‘The Black Butterfly’ na imetoka hivi karibuni na imesheheni nyimbo tano ambazo ni ‘Kilometa Ziro’, ‘Maringo’ ft Mimi Mars, ‘Shika’ ft Baba Levo, ‘Manyunyu’ ft Rosa Ree pamoja na ‘Ameniwahi’ ambayo amempa shavu Dogo Janja.

Soma Pia: Jay Melody Azungumzia Ripoti Kuwa Amejiunga na Lebo ya Rayvanny Next Level Music

Kwenye EP hii Mwasiti amegudia vitu tofauti kama maumivu ya kwenye mapenzi, furaha na pia kwenye wimbo wa ‘Maringo’ mwanamuziki ametoa mafunzo na elimu kubwa kwa mabinti wa kike kuhusu kujitunza.

Mwasiti anaingia kwenye orodha ya wasanii ambao wametoa EP kwa mwaka 2021 wengine ni pamoja na Lavalava, Quick Rocka, Man Fongo na wengineo wengi.

Leave your comment

Top stories

More News