Nyimbo Mpya: Linex Aachia EP Mpya ‘Tatu za Mjeda’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka  Tanzania Linex Sunday Mjeda hatimaye ameachia EP yake mpya ambayo ameipa jina la Tatu za Mjeda.

EP hiyo mpya imesheheni ngoma tatu ambazo ni ‘Malaika’, ‘Sina Cha Kupoteza’ akimshirikisha Darassa na ‘Sherehe’ aliyofanya na Belle 9.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Ngoma Yake Mpya ‘Outside’

Katika EP hii, Linex amejaribu kugusa aina tofauti za muziki huku akishirikiana na watayarishaji bora wa muziki kutoka Tanzania kama vile J Willz, T Touch na Papa.

Kwenye ngoma ya ‘Malaika’, Linex ameimba peke yake na ngoma hii ina vionjo vya pop. Kwemye wimbo huu Linex anamsifia mpenzi wake kwa mapenzi motomoto kiasi cha kumfananisha na malaika.

https://www.youtube.com/watch?v=HbvYQG_d5mY

Kwenye ngoma ya ‘Sherehe’ ambayo amemshirikisha Belle 9, Linex hakuwa na papara kwani ameimba kwa taratibu sana huku akielezea mipango aliyonayo na mpenzi wake. Belle 9 nae anatumia sauti kumsifia mpenzi wake huyo.

https://www.youtube.com/watch?v=RB_wOZ0eb5g

‘Sina cha kupoteza’ ni wimbo ambao Linex anakata tamaa ya kuwa na mpenzi kutokana na hali yake ya kimaisha kuwa duni. Linex anatawala sana kwenye aya ya kwanza huku Darassa akitema mashahiri kwenye aya ya pili.

https://www.youtube.com/watch?v=IrrIserSuRY

Leave your comment