Serikali ya Tanzania Yampongeza Rayvanny Kwa Kuandikisha Historia Kwenye Tuzo za MTV EMA
16 November 2021
[Picha: Rayvanny Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Serikali ya Tanzania chini ya wizara ya utamaduni, michezo na sanaa imempongeza mwanamuziki Rayvanny kwa kuandikisha historia kama msanii wa kwanza kutoka Tanzania kutumbuiza kwenye tuzo za MTV EMA ambazo zilifanyika nchini Hungary.
Ujumbe huo kutoka kwa serikali ya Tanzania una maana kubwa sana kwa wasanii wa bongo kwani ni ashirio kuwa serikali ipo tayari kuwashika mkono wasanii na kusherehekea mafanikio yao.
Soma Pia: Rayvanny Aweka Rekodi Baada ya Kutumbuiza Kwenye Tuzo za MTV EMA
"Tunampongeza Msanii Rayvanny kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kutumbuiza katika Tuzo za MTV EMMA za mwaka 2021 zilizofanyika Novemba 14, 2021 mjini BUDAPEST-HUNGARY," chapisho kutoka kwa wizara ya utamaduni, michezo na sanaa lilisomeka.
Rayvanny aliguswa na kutambuliwa na serikali ya nchi yake kama mwanamuziki ambaye alipeperusha bendera ya Tanzania katika hafla ya kimataifa.
Soma Pia: Harmonize Akataa Kulinganishwa na Msanii Yeyote, Aapa Kuibadilisha Tasnia ya Muziki
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Raryvanny aliandika ujumbe wa shukrani kwa serikali kwa kumuunga mkono katika taaluma yake ya muziki.
Alisema kuwa ni hisia nzuri na vile vile heshima kubwa kuona serikali ikitambua juhudi za wasanii.
"It feels so good when your government support your craft !! Thanks alot Ministry of Culture , arts and sports. Asante sana serikali yangu ya #tanzania hii ni heshima kwangu na sanaa kiujumla pale mnapotambua kile tunafanya watoto wenu . Asante sana wizara ya utamaduni, sanaa na michezo!" ujumbe wa Rayvany mtandaoni ulisomeka.
Leave your comment